Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ziara ya uongozi CCM nchini China kuimarisha ushirikiano

Ziara Ya Uongozi CCM Nchini China Kuimarisha Ushirikiano.jpeg Ziara ya uongozi CCM nchini China kuimarisha ushirikiano

Fri, 21 Apr 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Katibu Mkuu wa CCM, Ndugu Daniel Chongolo ameendelea na ziara kikazi nchini China huku akiongozana na viongozi wengine wa CCM, wakiwemo Wajumbe wa Sekretarieti ya NEC, Wenyeviti wa Mkoa pamoja na Wenyeviti wa Jumuiya.

Ziara ya Katibu Mkuu wa CCM inalengo la kuendeleza mahusiano ya Kirafiki na Kindugu yaliyopo kati ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) na Chama Cha Kikomonisti Cha China (CPC).

Pamoja na Mambo Mengine CCM na CPC zimejikita zaidi katika kusaidiana katika mambo ya Elimu na Mafunzo ya Falsafa ya Siasa na Uchumi. Mahusiano kati ya vyama hivi, yameasisiwa na waanzilishi wa vyama hivyo vikongwe na kuendelea kuimarishwa na viongozi wa sasa.

Ziara hii imeanza tarehe 16 Aprili, 2023 na inatarajiwa kumalizika tarehe 26 Aprili, 2023.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live