Katibu wa Siasa, Uenezi na Mafunzo wa Chama Cha Mapinduzi – CCM, Mkoa wa Morogoro Zangina Shanang Zangina, amejibu hoja zilizotolewa na Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Demokrasia na Maendelea – CHADEMA, Tundu Lissu wakati wa Maandamano Mkoani humo kwa madai ya kuwa anaipotosha umma.
Akizungumza na Wanahabari, Zangina, amesema hoja kubwa ya maandamano ya Chadema ni kutaka katiba kabla ya uchaguzi mkuu 2025 kwa maslai yao wenyewe na si kwajili ya wananachi.
“Nilikuwepo uwanjani nanikamsikia live kabisa akisema atuandamani kwasababu maisha magumu hapana hatuandamani kwasababu ya changamoto za wananchi hapana ,tunaandamana kwasababu ya katiba mpya,” alisema Zangina.
Ameongeza kuwa, baadhi ya Wananchi awana uelewa mzuri juu ya Katiba Mpya na ndio maaana wakiulizwa wanataka nini kiwe kwenye katiba hiyo awafahamu vyema.
“Wananchi walio chini wakiulizwa je unataka nini kiwe kwenye katiba mpya walio wengi watasema wanataka katiba iagize kushuka kwa mfumuko wa bei , nataka katiba mpya iagize kuondoka kwa manyanyaso katika hospitali na maeneo ya huduma za kijamii unapata picha kwamba kumbe huyu ajui kwenye katiba mpya kiandikwe kitu gani,” amesema Zangina.
Hata hivyo, Serikali inatakiwa kutoa Elimu zaidi kuhusu Katiba hili kusawaidia wanachi kuwa na uelewa mzuri lakini pia itaondoa sintofahamu iliyopo kwa jamii.