Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

ZITTO KABWE AVINYOSHEA KIDOLE VYAMA VYA UPINZANI

Zitto Kabwe?fit=800%2C445 ZITTO KABWE AVINYOSHEA KIDOLE VYAMA VYA UPINZANI

Wed, 19 Aug 2020 Chanzo: zanzibar24.co.tz

Kiongozi wa chama cha ACT Wazalendo Zitto Kabwe, amevitaka vyama vya upinzani nchini kuache ubinafsi kwa kuwa Tanzania ni kubwa kuliko vyama na Watanzania hawatowasamehe kama hawatoamua kuwa na mgombea mmoja wa Urais, Ubunge na Udiwani.

Zitto ameyasema hayo jana Agosti 18, 2020, Jijini Dar es Salaam na kuengeza kuwa mpaka sasa viongozi wanaendelea na mazungumzo kwa ajili ya vyama hivyo kushirikiana katika Uchaguzi Mkuu ujao na anaamini kuwa Watanzania wengi wanataka mashirikiano.

“Watanzania hawatatusamehe tusipokuwa na mgombea mmoja wa Urais, mgombea mmoja kila Jimbo,na kila Kata, wito wangu kwa viongozi wenzangu wa vyama vya upinzani tuache ubinafsi, Watanzania wanataka ushirikiano ili kuleta mabadiliko katika nchi, na joto la uchaguzi mmeliona watu wamechangamka Bara na Visiwani” amesema Zitto Kabwe.

Chanzo: zanzibar24.co.tz