Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

ZEC yatangaza uchaguzi jimbo la Pandani

Fb228d512c6ccabf3f12494c2f0ee7e6 ZEC yatangaza uchaguzi jimbo la Pandani

Sat, 19 Dec 2020 Chanzo: habarileo.co.tz

TUME ya Uchaguzi ya Zanzibar (ZEC) imesema uchaguzi mdogo wa nafasi ya uwakilishi jimbo la Pandani mkoa wa kaskazini Pemba utafanyika mwakani, Machi 28.

Taarifa ya Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar (ZEC) kwa vyombo vya habari imesema uchaguzi huo unafanyika kwa mujibu wa sheria wakati inapotokea dharura ikiwemo kifo na uchaguzi huo unatakiwa kufanyika si chini ya miezi minne.

Kwa mujibu wa taarifa uchaguzi huo utafanyika sambamba na wadi ya Kinuni na vyama vya siasa vimetakiwa kujipanga kushiriki katika uchaguzi huo.

Uchaguzi huo unafanyika kufuatia aliyekuwa mwakilishi mteule wa jimbo hilo Abubakar Khamis Bakary kufariki dunia mapema mwezi wa Novemba na hakuwahi kula kiapo cha kuwatumikia wananchi wa jimbo la Pandani.

Tayari baadhi ya vyama vya siasa vimesema vitashiriki katika mchakato wa uchaguzi huo ili kutimiza matakwa ya kidemokrasia ya mfumo wa vyama vingi.

Mwenyekiti wa Chama cha Ada Tadea, Juma Ali Khatib alisema tayari wamepokea taarifa kutoka kwa Tume ya Uchaguzi na wameanza kujipanga kushiriki uchaguzi huo mdogo.

“'Tume ya uchaguzi imetoa taarifa ya kufanyika kwa uchaguzi mdogo wa jimbo la Pandani na kuvitaka vyama hivyo kushiriki katika mchakato huo...tumeanza kujipanga,” alisema Khatib.

Mchuano wa kuwania jimbo la Pandani unatazamiwa kuwa kati ya Chama cha Mapinduzi (CCM) na chama cha ACT-Wazalendo.

Chanzo: habarileo.co.tz