Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Yatakayotugharimu upinzani Oktoba 28

4d9d3ea5d1229ae13a18f4f8cb047c42 Yatakayotugharimu upinzani Oktoba 28

Wed, 7 Oct 2020 Chanzo: habarileo.co.tz

VYOMBO vya Habari jana vilimkariri Katibu Mkuu wa CCM, Dk Bashiru Ally akivitaka vyama vya upinzani kujiandaa kisaikolojia kuanguka vibaya katika uchaguzi utakaofanyika Oktoba 28 mwaka huu hata kama vitaungana.

Alitoa sababu mbili za CCM kuibuka mshindi ambazo ni kuwa na wagombea makini na wanaokubalika pamoja na kubebwa na kazi nzuri iliyofanywa na chama hicho katika kipindi cha uongozi wa Rais John Magufuli.

Lakini upinzani pia utaanguka kwa sababu nyingine kadhaa kama ifuatavyo. Mosi, ni hatua yao ya kususia uchaguzi wa serikali za mitaa uliofanyika mwaka jana Novemba 24.

Uchaguzi wa serikali za mitaa ulikuwa msingi muhimu wa uchaguzi mkuu utakaofanyika tarehe 28 mwezi huu kwa vyama vya upinzani nchini. Katika uchaguzi huu muhimu, vipo vyama ambavyo vilijitoa katika kinyang’anyiro hicho.

Vyama vilivyotangaza kujitoa kushiriki uchaguzi huo ni Chadema, UMD, CCK, NCCR-Mageuzi, NLD, ACTWazalendo, CUF na Chauma kwa hoja ya kuenguliwa wagombea wa vyama vyao ambao hawakukidhi matakwa na vigezo vilivyoweka na Tume ya uchaguzi.

Wakati mwaka huu walioenguliwa kwenye vyama hivyo walikata rufaa lakini katika uchaguzi wa serikali za mitaa vyama viliamua kususa. Kususia uchaguzi huo kuna athari kuu tatu kwa vyama vya upinzani kwa uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika tarehe 28 Oktoba 2020.

Athari ya kwanza ni vyama vya upinzani kutopata somo lolote katika uchaguzi wa serikai za mitaa na hivyo kurekebisha makosa. Kwa mantiki hiyo ni rahisi kuweza kufanya hayo makosa kipindi hiki cha uchaguzi mkuu.

Athari ya tatu ni idadi kubwa ya wanachama wa vyama hivi kukata tamaa ya kujiandikisha kwa kuwa na mawazo kuwa yaliyotokea kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa, yaani kususia uchaguzi, yatatokea tena kipindi cha uchaguzi huu mkuu.

Hii imechangia pia vyama hivi kuwa na wagombea udiwani na ubunge wachache kulinganisha na CCM. Athari ya tatu ni kukosa wenyeviti wa kutosha wa serikali za mitaa ambao wana mchango mkubwa katika kuimarisha vyama na kuweza kuvipatia ushindi kutokana na majukumu yao katika kata.

Sababu ya pili itakayoviangusha vyama vya upinzani ni hofu ya kutoaminiana. Vyama vya upinzani vimekuwa vikipokea wanachama wa CCM na kuwapa nyadhifa kubwa za kimaamuzi katika vyama vyao lakini watu hawa wamelelewa katika utamaduni tofauti.

Viongozi hawa wamekuwa wakirejea ndani ya CCM wakiwa na siri kubwa za vyama vya upinzani baada ya kushindwa kukubaliana na sera za vyama hivyo. Hofu hii inasababisha pia utekelezaji wa majukumu ya vyama kuwa na usiri mkubwa na kutokuaminiana.

Hili limekuwa likizorotesha shughuli za vyama vya upinzani hasa kipindi hiki cha uchaguzi mkuu. Sababu ya tatu ni aina ya wafuasi wa vyama vya upinzani. Wafuasi wa vyama hivi wamekua wa aina tatu za watu.

Aina ya kwanza ni ile ya mafisadi na wahujumu uchumi ambao serikali ya awamu ya tano iliwadhibiti na aina ya pili ya wafuasi ni vijana wahuni waliokuwa wakinufaika na sera za utawala uliopita hii ni pamoja na wahalifu wachache ambao serikali ya awamu ya tano imewadhibiti.

Aina ya tatu ya wafuasi wa vyama hivi ni wanaharakati ambao wanatumiwa na mataifa ya nje kuihujumu Tanzania kwa maslahi yao. Sababu ya nne ya anguko la vyama vya upinzani ni wafuasi wao wengi kutokujiandikisha kupiga kura.

Ni wazi kuwa vyama vya upinzani vilikosa kuwahamasisha wafuasi wao kujiandikisha na kuhakiki taarifa zao kwenye daftari la wapigakura.

Msisitizo mkubwa uliwekwa kwenye suala la Tume huru ya uchaguzi huku viongozi wao wakitamka wazi kutoshiriki uchaguzi bila ya uwepo wa Tume huru ya

Chanzo: habarileo.co.tz