Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

YAJUE MAMBO TISA ALIYOZUNGUMZA JPM ZANZIBAR

Capture 404?fit=1046%2C696 YAJUE MAMBO TISA ALIYOZUNGUMZA JPM ZANZIBAR

Sun, 4 Oct 2020 Chanzo: zanzibar24.co.tz

Mgombea wa urais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dk.John Pombe Magufuli akiwa kwenye kampeni zake visiwani Zanzibar katika viwanja vya Mnazi mmoja hapo jana Oktoba 3 ,2020 alizungumza mambo mbali mbali na kuomba kura kwa wazanzibar.

Haya hapa ni mambo tisa aliyozungumza JPM kwenye hutuba yake hapo jana .

“Dkt. Hussein Mwinyi ni mkali, anafanana kidogo na Mimi ndio maana nampenda, nawaomba mumjaribu kwa miaka 5 halafu muniulize, asipofanya ninayosema kwavile nitakuwa bado Mwenyekiti wa CCM tutamuambia pumzika tutafute mwingine ila nina uhakika Mwinyi anatosha, Mwinyi anafaa kuwa Rais, mpeni kura nyingi”-JPM akiwa Zanzibar

“Amani ndio kila kitu, tumezingatia suala la Amani ndio maana nawaomba mumchague Hussein Mwinyi, amekuwa Waziri wa Ulinzi kwa miaka mingi, Uwaziri ameaminika hawezi kushindwa Urais, Wazanzibar nawaomba mumpe kura Hussein Mwinyi, nipeni kura Mimi na muwape kura Wabunge na Madiwani” -JPM

“Ukimsikia Mtu anasema Muungano hauna faida wakati Serikali ya Muungano imekopa Tsh. Trilion 2.3 kwa ajili ya Zanzibar pekee yake ujue huyo Mtu amepungikiwa kichwani, naomba tudumishe Muungano,pia Unguja na Pemba Mgawanyiko unatakiwa upotee, sisi ni Taifa moja”– JPM akiwa Zanzibar

“Nimejitokeza kugombea ili niutetee, kuulinda na kuudumisha Muungano, kwasababu kwenye Uchaguzi huu wamejitokeza Watu ambao kwa maneno yao, vitendo na hata sura zao na muonekano wao wanaonesha dhahiri kwamba hawapendi na hawautaki Muungano huu” -JPM

“Nitayalinda Mapinduzi matukufu ya Zanzibar, changamoto ndogondogo za Muungano tutazimaliza, hata mgogoro wa ZECO na TANESCO , ZECO ilikuwa inadaiwa zaidi ya Bilioni 22.9 nikalifuta Deni, kwasababu Zanzibar ni Tanzania na Tanzania ni Zanzibar”-JPM

“Nakuomba Dr.Hussen Mwinyi, ili nakuomba sikulazimishi, ukifanikiwa kuchaguliwa kuwa Rais wa Zanzibar, na Mimi kwasababu ni Kaka yako wa kuzaliwa, hakikisha Makamu wako wa pili wa Rais anatoka Pemba, nilitamani kwenda Pemba, nawaomba Wapemba wampe kura Mwinyi”-JPM akiwa Zanzibar

“Zanzibar vizuri hamuvijui, Pemba kulikuwa na Mbarawa kagombea wee wakamnyima, nikampa Wizara ya Ujenzi ambayo nimetoka huko, baadaye nikampeleka kuwa Waziri wa Maji hadi leo, ila Pemba hawamjui kuwa ile ni dhahabu, Wazuri mnawapiga vita badala ya kuwatumia”-JPM

”Asanteni sana Zanzibar, sijawahi kupata mapokezi kama haya mmevunja rekodi, naombeni kura, mpeni kura Hussein Mwinyi, Wabunge na Madiwani” JPM

“Unajua Rais Mstaafu Mzee Mwinyi aliniambia siri ya kuishi maisha marefu yeye ana miaka karibu 96 ni kuwa na Wanawake wawili, sasa mimi nina mmoja tu nikimaliza Urais nitaangaliaangalia kupata wa pili huku Zanzibar, nimeona mambo mazuri huku” -JPM 

Chanzo: zanzibar24.co.tz