Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wenyeviti wanne UWT Kilimanjaro waangushwa

Kilimanjaro Wenyevit Wenyeviti wanne UWT Kilimanjaro waangushwa

Sun, 25 Sep 2022 Chanzo: Mwananchi

Mkoa wa Kilimanjaro umepata viongozi wapya wa Umoja wa Wanawake wa Chama Cha Mapinduzi (UWT) katika wilaya saba za mkoa huo, ambapo wenyeviti wanne wilaya za Moshi vijijini, Hai, Same na Mwanga wameshindwa kutetea nafasi zao baada ya wajumbe kuwabwaga.

Wenyeviti walioshindwa kutetea nafasi zao ni aliyekuwa mwenyekiti wa Moshi Vijijini, Grace Mnzava aliyepata kura 109 na kuangushwa na Ruwaichi Kaale aliyepata kura 233, Wilaya ya Hai, Ester Sereya aliyepata kura 24 huku Hapiness Kimaro ambaye ni mshindi akipata kura 184.

Wilaya ya Same, Stella Mramba aliyepata kura 99 na Mwajuma Mgonja akiibuka .shindi kwa kupata kura 324.

Akizungumza na Mwananchi Digital, jana Jumamosi, Septemba 24, 2022, Katibu wa UWT, Mkoa wa Kilimanjaro, Irimina Mushongi amesema uchaguzi katika ngazi ya Wilaya umekamilika kwa asilimia 100 mkoani humo.

Amewataja wenyeviti waliochaguliwa  ni Theresia Komba (Moshi Mjini), Hapiness Kimaro (Hai), Better Isaka (Siha), Amina Mrengwe (Mwanga), Ruwaichi Kaale (Moshi Vijijini), Mwajuma Mgonja (Same) na Angelia Mtenga (Rombo)

“Tunamshukuru Mungu tayari tumekamilisha uchaguzi katika wilaya zote Mkoa wa Kilimanjaro, niwapongeze wote waliochaguliwa, sasa ni mwendo wa kazi katika kukipigania chama cha mapinduzi na kuhakikisha kinaendelea kushika dola," amesema

Related Mwenyekiti UWT Kilosa aanguka, mpya aeleza vipaumbele Diwani wa zamani Chadema ashinda UWT, mpinzani wake asema...Advertisement Akizungumza mwenyekiti wa Moshi vijijini, Kaale baada ya kutangazwa Mshindi, amewaahidi kina mama kuanzisha miradi mbalimbali ya kiuchumi ya umoja huo ili kuwezesha umoja kujitegemea.

Chanzo: Mwananchi