Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wenje: CHADEMA tukichukua madaraka tunawafuta Ma-DC wote!

Wenje CHADEMA.jpeg Wenje: CHADEMA tukichukua madaraka tunawafuta Ma-DC wote!

Tue, 18 Apr 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Kanda ya Victoria, Ezekia Wenje amesema mfumo wa utawala uliopo nchini unachangia viongozi kufanya ubadhirifu wa mali za Umma huku akidai utawala wa majimbo utasaidia kukabiliana na changamoto hiyo.

Pia amesema utawala wa majimbo ambao ni kipaumbele cha Chadema utasaidia kutatua kero za wananchi kwa wakati ikilinganishwa na sasa ambapo waziri mmoja anaongoza wizara nchi nzima jambo alilodai linachelewesha huduma kwa wananchi.

Wenje ambaye ni Mbunge mstaafu wa Jimbo hilo amesema hayo jana Jumatatu Aprili 17, 2023 wakati akihutubia wananchi wa Jiji la Mwanza katika eneo la Mirongo na kuwataka wananchi kutofanya makosa katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa (2024) na Uchaguzi Mkuu (2025).

Chanzo: www.tanzaniaweb.live