Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Waziri Mkuu acharuka, atoa siku tano Wizara ya Kilimo

Screenshot 20220608 152942 Chrome Waziri Mkuu

Wed, 8 Jun 2022 Chanzo: Tanzania

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa ametoa siku tano kuanzia leo Juni 8, 2022 hadi Juni 12, 2022 Wizara ya Kilimo iwe imeondoa pikipiki zote wizarani hapo na kuzikabidhi kwa wakurugenzi.

“Hii haikubaliki, Wakurugenzi wote waandikiwe barua waje wazichukue, kama kuna ufungaji wa plate number utafanyika huko huko. Jumapili saa 10 jioni ziwe zimefika kwa wahusuka.”

Ametoa agizo hilo leo Juni 8, 2022 alipokagua Ofisi za Wizara ya Kilimo zilizopo eneo la VETA, Dodoma na kukuta pikipiki zilizotolewa kwa ajili ya maafisa ugani zikiendelea kuwepo.

Chanzo: Tanzania