Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Waziri Mhagama, Dk Fereshi wampisha kiti Dk Biteko bungeni

Waziri Mhagama, Dk Fereshi Wampisha Kiti Dk Biteko Bungeni Waziri Mhagama, Dk Fereshi wampisha kiti Dk Biteko bungeni

Mon, 4 Sep 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Jenista Mhagama, pamoja na Mwanasheria Mkuu wa Serikali Dk Eliezer Feleshi wamelazimika kuhama kwenye nafasi zao walizokuwa wakikaa awali bungeni na kumpisha Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk Dotto Biteko.

Waziri Mhagama na Dk Feleshi awali walikuwa wanakaa kwenye mstari mmoja wa viti vya mbele pamoja na Waziri Mkuu.

Dk Biteko aliingia bungeni kwa mara ya kwanza baada ya kuapishwa katika nafasi hiyo leo Jumatatu Septemba 4, 2023 na alipoingia hakukaa kwenye kiti cha Waziri Mkuu badala yake alienda moja kwa moja kwenye eneo hilo.

Hivyo, mstari ambao Dk Biteko amekaa leo una viti vinne, kimoja ni cha Waziri Mkuu pamoja na cha ziada kwaajili ya Wabunge wanaokwenda kuzungumza naye akiwa bungeni.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live