Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wazee wa Chadema watoa neno kwa Serikali ya Tanzania

78016 Pic+chadema+wazee

Wed, 2 Oct 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Baraza la wazee la chama kikuu cha upinzani nchini Tanzania cha Chadema limesema wazee wa nchi hiyo wanapaswa kutungiwa sheria za kuwalinda na kusimamia ustawi wao kama ilivyo kwa makundi mengine.

Baraza hilo limeeleza hayo leo Oktoba 1, 2019 ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya siku ya wazee duniani ambayo huadhimishwa tarehe kama ya leo kila mwaka.

Makamu Mwenyekiti wa Baraza hilo, Suzan Lyimo amesema Serikali ya Tanzania inapaswa kupeleka muswada bungeni ili kutunga sheria inayosimamia huduma bora kwa wazee na uwezeshwaji kiuchumi kwa kuwaweka kuwa wanufaika wa asilimia 10 ya mapato ya halmashauri kama ilivyo vijana na walemavu.

"Wazee ni watu ambao wana mchango mkubwa katika jamii ya sasa lakini wamekuwa hawathaminiwi, Serikali inapaswa kutunga sheria ya kuwalazimisha watoto kuwalea wazee wao kama ambavyo wazazi wanalazimishwa na sheria kuwatunza watoto," amesema Lymo.

Amesema katika hospitali licha ya kuwa kuna wazee wana kadi za kutibiwa bure lakini kunapaswa kuwa na dirisha maalumu ili waweze kupata huduma bora na haraka.

Naye Mwenyekiti wa Baraza hilo, Hashim Juma Issa amesema watashawishi kamati kuu ya chama hicho kujali wazee kwa kuweka mpango huo katika ilani ya uchaguzi wa chama.

"Chadema tunataka tukiingia madarakani tuwe na agenda ya kuwajali wazee, tunataka kuwa na viti maalumu bungeni kwa ajili ya wazee na kuwa na baraza la wazee kitaifa ambalo litasaidia kukomboa wazee," amesema Issa.

Chanzo: mwananchi.co.tz