Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wazee wa CCM wataka Rais Samia asisumbuliwe 2025

Samia Ccm.jpeg Rais Samia Suluhu Hassan

Thu, 8 Dec 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Wazee wa Chama cha Mapinduzi (CCM) wamewataka wajumbe wa Mkutano Mkuu wa 10 wa chama hicho kuazimia kwa sauti moja kuwa Mwenyekiti wa chama hicho, Rais Samia Suluhu Hassan ndiye atakaye kuwa mgombea wa CCM katika Uchaguzi Mkuu wa 2025.

Mzee Yusuf Makamba amesema kuwa Dk Samia ni chaguo sahihi na kwamba kama wajumbe waache unafiki kwa kupitisha azimio ambalo amesema litaondoa mianya ya baadhi ya wana-CCM kuweka nguvu kutafuta mgombea ama kuvuruga mgombea.

“Niseme tu, Ndugu Katibu MKuu (Daniel Chongolo) usiogope kuhusu utaratibu ama Katiba. Huo utaratibu na hiyo Katiba tumeiandika sisi wenyewe kama tunavunja utaratibu kwa nani? Hio kama ni tatizo tuibadili Rais Samia isimame 2025 tuazimie hilo hapa,” amesema Mzee Makamba.

Mwenyekiti wa Kamati ya Maazimio, Ndugu Mizengo Pinda hata hivyo hakuweza kutaja hilo kama sehemu ya maazimio ya kikao hicho.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live