Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wazee Chadema waeleza watakavyomshauri Rais

35253 Pic+wazee Baraza la Wazee la Chadema

Wed, 9 Jan 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Baraza la Wazee la Chadema limesema endapo mgombea wa chama hicho ataibuka na ushindi katika uchaguzi mkuu wa 2020, baraza hilo litakuwa na jukumu la kumshauri, kuamua masuala ya msingi ya Taifa.

Kauli hiyo imetolewa leo Jumatatu Januari 7, 2019 na mwenyekiti wa baraza hilo, Hashim Issa Juma katika mkutano na waandishi wa habari, wakati akieleza upungufu wa Serikali kwa sasa katika kuongoza nchi.

Juma amesema baraza hilo litakaloundwa na wajumbe zaidi ya 100 litakuwa na nguvu zaidi ya kuamua masuala ya nchi badala ya Rais.

"Halafu kila baada ya miezi mitatu tutakuwa tunakutana na Rais wa nchi kumpatia maelekezo na kumshauri. Rais hatakuwa na nguvu yoyote, ila sisi wazee tutakuwa na wizara maalumu ya kushughulika na wazee nchini, "amesema Juma.

Katika hatua nyingine, wazee wa baraza hilo wameitaka Serikali na vyombo vya dola kuhakikisha inaendesha Taifa kwa misingi ya haki na sheria za nchi, huku wakilaani matukio ya ukandamizaji wa demokrasia unaolenga kuua upinzani nchini Tanzania.



Chanzo: mwananchi.co.tz