Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wazee ACT-Wazalendo waweka msimamo uchaguzi Serikali za mitaa

Sun, 7 Jul 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Ngome ya wazee ya chama cha ACT- Wazalendo imesema itashirikiana na vyama vingine vya siasa kuhakikisha atakayeshinda katika uchaguzi wa Serikali za mitaa nchini Tanzania anatangazwa.

Hayo yameelezwa leo Jumamosi Julai 6, 2019 na mwenyekiti wa ngome hiyo, Yeremia Maganja katika ufunguzi wa kikao cha kikosi kazi kuelekea uchaguzi wa huo utakaofanyika Oktoba 2019.

Katika kikao hicho kilichowahusisha wazee kutoka Mikoa mbalimbali nchini, Maganja amesema kwa sasa kuna shida ya kutofuatwa kwa misingi ya katiba na sheria katika chaguzi.

"Tutashirikiana na vyama vingine pamoja na wananchi kueleza kuhusu kuheshimu katiba na kufanya kazi kwa mujibu wa sheria ili atakayeshinda atangazwe,” amesema  Maganja

Amedai wagombea wa vyama vya upinzani wamekuwa wakiibuka na ushindi katika chaguzi lakini hawatangazwi.

"Sisi kama viongozi wa vyama tutahakikisha inapatikana tume huru ya uchaguzi ili atakayeshinda atangazwe na  tutahakikisha hili linatekelezeka,” amesisitiza.

Pia Soma

Katibu wa Ngome ya wazee,  Hamadi Tao amesema pamoja na kupanga mikakati kuelekea uchaguzi watapitia upya  kanuni zinazotumika kuiongoza ngome hiyo.

 

Chanzo: mwananchi.co.tz