Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wazazi CCM wampongeza Magufuli kuingilia kati kikokotoo

34725 CCM+pic Tanzania Web Photo

Fri, 4 Jan 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Jumuiya ya Wazazi CCM imempongeza Rais John Magufuli kumaliza mjadala uliotokana na kanuni mpya za Sheria ya Hifadhi ya Mifuko ya Jamii ya mwaka 2018, baada ya kuamuru utumike utaratibu wa zamani katika kipindi alichokiita cha mpito hadi mwaka 2023.

Rais Magufuli aliagiza kurejeshwa kwa utaratibu wa zamani wa wastaafu serikalini wa kupewa mafao ya mkupuo ya asilimia 50 badala ya asilimia 25 iliyopendekezwa katika kanuni hizo mpya.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Alhamisi Januari 3, 2019 mwenyekiti wa jumuiya hiyo, Dk Edmund Mndolwa amesema uamuzi huo umelenga kuhakikisha wafanyakazi Tanzania wanaendelea kutazamwa vyema hata watakapostaafu.

“Wazazi CCM tunampongeza mwenyekiti wa CCM (Rais Magufuli) kwa busara yake ambayo imerudisha imani ya wastaafu. Jambo hili lilileta sintofahamu iliyozua mjadala mkubwa. Wazazi tunampongeza kwa kuahirisha mchakato huo mpaka mwaka 2023 ili wadau wa mifuko hii waweze kujadiliana kwa kina kwa faida ya pande zote mbili,” amesema.

“Jambo hili ni muhimu sana kwa sababu litafanya sasa mjadala huu uwe wa wazi zaidi ili uamuzi utakaotoka baada ya kipindi hiki cha mpito cha majadiliano uwe kwa maslahi ya wote.”



Chanzo: mwananchi.co.tz