Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Watoto wa Nyerere washindwa kura za maoni Butiama

JK Kids Watoto wa Mwalimu Nyerere

Tue, 21 Jul 2020 Chanzo: millardayo.com

Watoto wa Mwalimu Julius Nyerere, Makongoro na Madaraka, wamepata kura chache katika kura za maoni Jimboni kwao Butiama, Mara.

Jimbo la Butiama lilikuwa na wagombea 59 na wajumbe waliopiga kura walikuwa 555 na matokeo yaliongozwa na Jumanne Sagini aliyepata kura 84, akifuatiwa na Frank Mahemba aliyepata kura 80, wa tatu akiwa Joseph Nyamboha kura 46.

Katika kura hizo za maoni Makongoro Nyerere alipata kura 5 na Madaraka Nyerere aliambulia kura 2. Makongoro Nyerere aliwahi kuwa Mbunge wa Arusha kupitia NCCR-Mageuzi.

BREAKING: NDUGULILE AIBUKA KIDEDEA KIGAMBONI, MAKONDA APIGWA CHINI KURA ZA MAONI

Chanzo: millardayo.com