Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Watia nia ubunge, udiwani CCM watakiwa kuwa watulivu

B9516f0aa598eb1bf643987241686a99 Watia nia ubunge, udiwani CCM watakiwa kuwa watulivu

Wed, 19 Aug 2020 Chanzo: habarileo.co.tz

MJUMBE wa Halmashauri Kuu ya Chama cha Mapinduzi(CCM) Taifa Mussa Mwakitinya amewataka watia nia wa nafasi za Ubunge na udiwani ndani ya chama hicho kuwa wavumilivu wakati huu ambapo vikao vya chama vinaendelea kufanya mchujo wa wagombea.

Akizungumza jana na Jumuiya ya wanafunzi wa Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TaSUBa) alisema wanachama wote wa chama hicho wanalo jukumu la kuhakikisha kuwa wanakilinda chama chao dhidi ya aina yoyote ya hujuma za kisiasa kutoka kwa watu wenye dhamira mbovu.

Alisema wakati huu ambao chama hicho kinaendelea na mchakato wake wa kuwatafuta wagombea wenye sifa sahihi za kuhakikisha majimbo mbalimbali kwa ajili ya uchaguzi mkuu ujao, wanapaswa kuwa watulivu kwa lengo la kuijengea heshima chama hicho.

"Ni vyema wawania wakawa watulivu na ikibidi wawepo katika majimbo yao kama ambavyo Katibu Mkuu wetu ameagiza, ukweli ni wazi kuwa chama chetu pamoja na kiongozi wake wapo makini katika tekeleza majukumu yao" alisema Mwakitinya

Aidha alisema huu ni wakati muafaka kwa wanachama wa chama hicho kukipigania chama chao ikiwa ni pamoja na kupambana wale wote wanaoshusha heshima ya chama hicho na Rais John Magufuli.

Alisema wapo baadhi ya watu wanaotumia mitandao na kukichafua chama hicho ambapo amewataka wanafunzi hao kutumia busara kwa kuwajibu kwa kutumia vigezo vya maendeleo yaliyofanywa na chama hicho.

Alisema hawapaswi kuwajibu watu hao kwa kuzingatia utafiti unaotokana na taaluma walizonazo huku akisisitiza kuwa CCM siyo siyo chama chenye tabia ya kukurupuka kwa kuongea mambo yasiyo na tija.

Chanzo: habarileo.co.tz