Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Watatu CUF Tanga, wavuliwa udiwani

11144 Cuf+pic TanzaniaWeb

Tue, 10 Jul 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Mkurugenzi wa Jiji la Tanga Daudi Mayeji ametangaza kuwavua udiwani madiwani watatu wa CUF mkoani humo baada ya kupelekewa barua ya kuvuliwa kwao uanachama na naibu katibu mkuu wa chama hicho bara, Magdalena Sakaya.

Madiwani hao ni Rashid Jumbe wa kata ya Mwanzange, ambaye ndiye Mwenyekiti wa CUF wilaya ya Tanga, mwingine ni Fatma Hamza (Viti Maalum) na Halima Mbwana (Viti Maalum.)

Sakaya alipeleka barua hiyo ya kuwavua uanachama madiwani hao Ijumaa wiki iliyopita kwa kile alichosema walikataa kuweka mgombea katika kata ambazo zilibaki wazi baada ya madiwani wa CUF kuhamia CCM.

“Wale madiwani akiwamo mwenyekiti wa CUF wilaya ya Tanga, walikataa kuweka mgombea maeneo ambapo madiwani wetu walihamia CCM, wakaanza malumbano, wakisema wamepewa maagizo tuweke wagombea wa Chadema,” amesema.

Amesema mwenyekiti huyo ambaye ni diwani wa kata ya Mwanzange na wenzake wawili wanaomuunga mkono nao walionywa na kupewa barua ya kujieleza wakakataa, ndipo wakavuliwa uanachama.

“Hatuwezi kuvunja katiba bila sababu za msingi, chama kinaongozwa kwa katiba. Inashangaza mtu kukataa kuweka mgombea wa chama chako na kulazimisha awekwe wa chama kingine,” amesema Sakaya.

Akizungumzia tukio hilo, Mayeji amesema amepokea barua hiyo jana na iliandikwa Juni 7.

Mayeji amesema barua ya CUF imetaja sababu za kuwavua uanachama madiwani hao kuwa ni kukivuruga chama kwa makusudi, kukaidi wito wa baraza la uongozi na kosa la tatu ni kuwavuruga wanachama wa CUF.

 

 

Chanzo: mwananchi.co.tz