Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wataokatwa CCM kujulikana wiki hii

D381115bb53a9bc885868502d3ef1390 Wataokatwa CCM kujulikana wiki hii

Mon, 17 Aug 2020 Chanzo: habarileo.co.tz

MAJINA ya wanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) watakaoteuliwa kugombes ubunge kwenye Bunge la Tanzania na uwakilishi katika Baraza la Wawakilishi Zanzibar yanatarajiwa kufahamika wiki.

CCM imetoa ratiba ya vikao vya uteuzi wa wabunge na wawakilishi kwa ajili ya Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba 28, mwaka huu.

Kwa mujibu wa ratiba hiyo, vikao hivyo vya kuchekecha majina vinaanza leo. Kikao cha Sekretarieti ya Halmashauri Kuu kitaketi kesho na pia kitafanyika kikao cha Kamati ya Usalama na Maadili ya Taifa.

Agosti 20 hadi 21 kitafanyika kikao cha Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa na Agosti 22 Jumamosi kitafanyika kikao cha Halmashauri Kuu ya Taifa.

Mchakato wa utangazaji nia kuwania kukiwakilisha chama hicho kwenye Uchaguzi Mkuuu umeweka historia kutokana na wingi wa wagombea kwa kuwa katika baadhi ya majimbo zaidi ya wanachama 100 walichukua fomu.

Dirisha la kuchukua fomu kwa nafasi za ubunge, udiwani na uwakilishi kwa chama hicho, lilifunguliwa Julai 14 hadi 17.

Baada ya hapo vilifanyika vikao vya ndani vya kamati za siasa za kata, jimbo na mkoa kujadili na kupitisha majina ya watakaowakilisha chama hicho kwenye uchaguzi.

Katika kura hizo za maoni majina makubwa wakiwemo mawaziri wa zamani na sasa, wakuu wa mikoa, vigogo wa Serikali na binafsi walianguka huku mawaziri waliopata ubunge kwa kuteuliwa na Rais kupitia nafasi 10 kwa mujibu wa Katiba ya Tanzania waking’ara.

Katibu wa Itikadi na Uenezi CCM Humphrey Polepole alisema kura za maoni si mwisho wa mchakao wa kupata wagombea kwa kuwa vikao vya juu vitafanya uamuzi wa mwisho

Polepole alisema, CCM itawashangaza na kuwashikisha adabu wagombea walioshiriki kwenye vitendo vya rushwa.

Chanzo: habarileo.co.tz