Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Watanzania watakiwa kuutunza Muungano

42159 Ccmpic Watanzania watakiwa kuutunza Muungano

Mon, 18 Feb 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Unguja. Wananchi wa Zanzibar na Watanzania kwa ujumla wametakiwa kuutunza na kuuenzi Muungano kati ya Tanzania bara na Zanzibar.

Hayo yemesemwa na naibu katibu mkuu CCM Zanzibar, Dk  Juma Abdalla Mabodi, leo Febuari 16, 2019 wakati wa sherehe maalumu ya kuwapongeza wanafunzi waliofanya vizuri katika mitihani yao ya kidato cha nne.

Amesema wasomi wa sasa wanapaswa kutambua ukweli kuhusu umuhimu wa Muungano na kukataa kabisa kudanganywa na watu aliowataja kuwa wenye nia mbaya kwa maslahi yao.

Mabodi amesema marehemu Mzee Karume aliingiza Zanzibar kwenye Muungano kutokana na umuhimu wa kufanya hivyo na si kwa lengo jengine na hadi leo hii wananchi wa pande zote mbili wanajivunia uwepo wa Muungano huu.

Amesema Muungano ndio ulioleta uhuru na kuwafanya wananchi wa pande zote mbili kujitawala na kuwa huru katika nchi yao.

Aliwataka wananchi wote kukataa na kutokubali chuki na fitna zinazoendelezwa kwa lengo la kuubeza Muungano kati ya Zanzibar na Tanzania bara.

 

 



Chanzo: mwananchi.co.tz