Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Watakiwa kuvunja makundi ya siasa za kampeni

0dcb115802abb5deac0b06ae38393d77.png Watakiwa kuvunja makundi ya siasa za kampeni

Wed, 25 Nov 2020 Chanzo: habarileo.co.tz

WANANCHI wa Mtaa wa Chinyoyo katika Kata ya Kilimani jijini Dodoma, wametakiwa kuvunja makundi waliyokuwa nayo wakati wa kampeni za Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2020 na badala yake, waungane kufanya kazi kwa juhudi na maarifa ili kuiletea maendeleo kata yao na taifa kwa jumla.

Mwenyekiti wa Mtaa wa Chinyoyo, alitoa mwito huo wakati akielezea mafanikio ya mtaa huo kwa kipindi cha miaka mitano iliyopita.

Alisema sasa ni wakati wa kuvunja makundi ya kisiasa waliyokuwa nayo wananchi katika kipindi kampeni za uchaguzi mkuu uliopita kuchagua rais, wabunge na madiwani.

“Watu sasa wavunje makundi ya kampeni na badala yake, waungane na kuwa kitu kimoja ili waendelee na shughuli za kuleta maendeleo yao binafsi na maendeleo ya kata,” alisema.

Mintarafu maendeleo katika kipindi cha miaka mitano iliyopita, alisema anajivunia ushirikiano na wananchi uliowawezesha kufikia maendeleo kadhaa yakiwamo ya upimaji wa ardhi.

"Pia kwa kufanya maboresho kwa mtaa wangu ambao tangu tupate uhuru, ulikuwa haujapimwa; wananchi walikuwa wakiishi hawajui hatma yao, lakini kwa ushirikiano wa serikali na wajumbe wa serikali ya mtaa ambayo mimi ni mwenyekiti na mbunge wa Dodoma Mjïni, Anton Mavunde na Kamati ya makazi ya mtaa na ofisi ya mkurugenzi kwa pamoja tumefanikisha ndoto ya muda mrefu," alisema.

Alisema kwa sasa wananchi wanaishi kwa amani na wanaweza kupata mikopo katika taasisi za kifedha baada ya kupimiwa ardhi katika maeneo yao na kuweza kujenga nyumba za kisasa zinazoendana na hadhi ya Jiji la Dodoma.

"Katika upimaji tumetenga eneo la kujenga shule ya sekondari na msingi za kata, pia tumetenga eneo la kujenga zahanati, soko, stendi na kituo cha polisi cha kata, hivyo Kata ya Kilimani itapata huduma zote za kijamii katika Mtaa wa Chinyoyo hasa ikizingatiwa kuwa, Kata ya Kilimani ndipo wanapokaa viongozi wengi wa kitaifa," a?isema.

Chanzo: habarileo.co.tz