Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wasimamizi wahadharishwa kuhusu maambukizo corona

NEC TZ Wasimamizi wahadharishwa kuhusu maambukizo corona

Fri, 1 May 2020 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

OFISA Mwandikishaji wa Jimbo la Iringa Mjini ambaye ni Mkurugenzi wa Manispaa, Hamid Njovu, amewataka wasimamizi wasaidizi ngazi ya kata na waandishi wasaidizi kutokuwa chanzo cha maambukizo ya ugonjwa wa corona.

Alisema hayo jana wakati akifungua mafunzo ya wasaidizi ngazi ya kata na waandishi wasaidizi, mjini hapa.

Njovu alisema katika uboreshaji daftari la wapigakura awamu ya pili ya uandikishaji, suala la mapambano dhidi ya virusi vya corona limezingatiwa kwa dhati na kutoa wito wa kuhakikisha wanajua utaratibu unaotakiwa katika mchakato mzima wa uchaguzi.

Alisema, madhumuni ya mafunzo hayo ni kuhusu uandikishaji wa wapigakura katika daftari la kudumu na uboreshaji wa wapigakura awamu ya pili ambao utafanyika katika vituo 18 vilivyopo kwenye kata katika Manispaa ya Iringa.

Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) ipo mkoani Iringa kwa ajili ya uandikishaji wapigakura katika daftari la kudumu na uboreshaji wa wapigakura awamu ya pili na kwa Manispaa ya Iringa utafanyika katika vituo 18 kuanzia Mei 2 hadi 4, mwaka huu.

“Ninaomba nitumie nafasi hii kuwakumbusha tena juu ya unyeti wa jukumu la kuwaelekeza wapigakura kuwa ni muhimu sana kuwaelewesha wananchi kutumia haki yao ya kupiga kura kwa kuzingatia maelekezo ya Tume ya Uchaguzi kikamilifu,” alisema Njovu.

Pia, aliwakumbusha kuwa uchaguzi ukivurugika madhara ni yake ni makubwa kwa amani ya nchi na ni madhara ya muda mrefu na pia ni hasara kwa taifa kwa kuwa serikali inatumia fedha nyingi katika uchaguzi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live