Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wasifu wa Mzee Mangula huu hapa

Phillipo Phillip Mangula akiwa katika moja ya majukumu ya Chama

Thu, 31 Mar 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Tanzania Bara, Philip Mangula (81) leo Alhamisi Machi 31, 2022 amewasilisha katika Halmashauri Kuu ya CCM barua ya kuachia nafasi hiyo.

Ufuatao ni wasifu wa kada huyo mkongwe na kindaki ndaki wa Ccm

KUZALIWA:

NDUGU Philipo Japhet Mangula , alizaliwa Tarehe 31 Machi 1941 katika kijiji cha Imalimnyi, Wilaya ya Wanging'ombe, Mkoa wa Njombe.

ELIMU NA MAFUNZO MBALIMBALI:

Mwaka 1950-1953 Alisoma katika Shule ya Msingi Kidugala, Wilaya ya Wanging'ombe,Mkoa wa Njombe.

Mwaka 1954-1957 Alisoma Shule ya Kati 9Middle School) ya Bulogwa Wilayani Makete.Mwaka 1957 alihamia Shule ya Kati ya Mpwapwa alipomiazia elimu yake ya darasa la Nane.

Mwaka 1958-1959 Alisoma Shule ya Sekondari ya Mpwapwa Mkoani Dodoma.

Mwaka 1960-1961 Alisomea Ualimu katika Chuo cha Ualimu Mpwapwa Mkoani Dodoma.

Mwaka 1966 April-Dec Alihuduria kozi ndefu ya masuala ya Siasa na Uongozi katika Chuo cha TANU, Kivukoni.

Mwaka 1967 Jan-Machi Alihudhuria mafunzo ya Kijeshi katika kambi y ajeshi la kujenga Taifa, Mgulani.Hiyo ilikuwa Operesheni Azimio.

Mwaka 1967 April-Juni, alirudi tena katika Chuo cha TANU Kivukoni kwa ajili ya Mafunzo Maalumu ya Ualimu wa Siasa. Baada ya mafunzo hayo aliteuliwa kuwa Mwalimu wa Siasa katika Mkoa wa Iringa.

Mwaka 1973-1976 Alisoma Chuo Kikuu cha Nairobi, Kenya na kuhitimu katika fani ya Mawasiliano ya Umma (Mass Communication).

KAZI NA MAJUKUMU MBALIMBALI

Mwaka 1962-1964 Alikuwa Mwalimu wa Shule ya kati (Middle School) ya Ntaba, Wilaya ya Rugwe, Mkoani Mbeya.

Mwaka 1965 Jan-Dec. Alikuwa Mwalimu wa Shule ya kati ya Mano, Wilaya ya Rugwe, Mkoani Mbeya.

Mwaka 1966 Jan-April Alikuwa Mwalimu wa Shule ya Msingi ya Gangilonga, Iliyoko Iringa Mjini.

Mwaka 1967 July-Dec Alikuwa Mwalimu wa Siasa katika Mkoa wa Iringa.

Mwaka 1968-1977 Alikuwa Mwalimu wa Siasa katika Chuo cha TANU, Kivukoni.Katika kipindi hicho alishika nyadhifa mbalimbali Chuoni hapo zikiwemo:-

Mkuu wa Idara ya Propaganda

Mwendeshaji kipindi cha Elimu ya Umma Radioni kilichojulikana kama FIMBO YA MNYONGE

Mhariri wa Majarida ya MBIONI,UJAMAA pamoja na Jarida Maalumu lililotolewa kwa lugha ya kiingereza ili kuhamasisha harakakati za Ukombozi Kusini mwa Afrika,lililokuwa likiitwa THE RATIONAL CHOICE.

Mwaka 1971,Aliteuliwa kwenda mstari wa mbele katika Jimbo la Cabo Delgado Msumbiji kushuhudia vita ya Ukombozi nchini humo.

Mwaka 1977-1983 Aliteuliwa kuwa Katibu wa CCM wa Wilaya na Mkuu wa Wilaya ya Kwimba, Mkoani Mwanza.

Mwaka 1983-1986 Aliteuliwa kuwa Makamu wa Mkuu wa Chuo cha CCM Kivukoni na Mkuu wa Mafunzo Chuoni hapo.

Mwaka 1986-1991 Aliteuliwa kuwa Katibu wa CCM wa Mkoa na Mkuu wa Mkoa wa Mwanza.

Mwaka 1992-1996 Aliteuliwa tena kuwa Katibu wa CCM wa Mkoa na Mkuu wa Mkoa wa Kagera.

Mwaka 1996-2006 Alichaguliwa kuwa Katibu Mkuu wa CCM.

Katika Kipindi chote hicho,Ndugu Mangula alisimamia kazi za Chama za Utendaji kwa umakini, umahiri, uhodari na uadilifu wa hali ya juu.

Ndugu Mangula akiwa ndiye mkurugenzi Mkuu wa uchaguzi ndani ya Chama, alisimamia kwa ustadi mkubwa kampeni za uchaguzi Mdogo wa Ubunge katika amjimbo 31 nchini, ambapo kati ya majimbo hayo CCM ilipoteza majimbo mawili tu.

Aidha, Ndugu Mangula aliteuliwa na Halmashauri Kuu ya Taifa kuwa Mwenyekiti wa kamati ya Kitaifa ya Kampeni za CCM kwa ajili ya Uchaguzi Mkuu 2000 na akateuliwa tena kufanya kazi hiyo hiyo mwaka 2005.Katika Chaguzi hizo CCM ilishinda kwa kishindo.

Ndugu, Philipo Japhet Mangula amekuwa Mjumbe wa Halmashauri kuu ya Taifa ya CCM kuanzia Mwaka 1984 alipochaguliwa kwa mara ya kwanza hadi 2007 ambapo aliamua kurudi kijiji kwake na kuwa Mkulima.

Hatimaye, Leo Machi 31 amewasilisha barua ya kupumzika akiwa na umri wa miaka 81.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live