Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Warioba: Msiujadili muungano kwa maslahi ya madaraka

Wariobaa12 Warioba: Msiujadili muungano kwa maslahi ya madaraka

Fri, 19 Apr 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

WAZIRI Mkuu na Makamu wa Kwanza wa Rais Mstaafu, Jaji Joseph Warioba amewataka viongozi wa serikali na wale wa vyama vya siasa kuacha kujadili muungano kwa kutazama manufaa yao kimadaraka badala yake wajikite zaidi kutatua changamoto za wananchi ili kuwaletea maendeleo.

Jaji Warioba ameeleza hayo leo jijini Dar es Salaam, katika mahojiano maalumu na waandishi wa habari, kuelekea Maadhimisho ya Miaka 60 ya Muungano.

"Mwananchi wa kawaida haangalii nani ana madaraka, anachotaka ni maendeleo. Tuangalie yatakayoimarisha muungano na sio madaraka," amesema na kuongeza kuwa kama viongozi watajikita kutatua mahitaji ya wananchi, migogoro yote itaisha.

"Upande wa huduma ya afya, Mtanzania anataka huduma ya aina moja, mfano, bima ya afya iwe inatumika Bara na visiwani," amesema.

Kuhusu kero za Muungano amesema: "Kero kwangu ni changamoto za maisha ya kila siku, ambayo hakuna siku zitakuja kwisha. Badala ya kuconcentrate kwenye maendeleo, yanaangaliwa mambo ya madaraka na siasa."

Amesema, ni wajibu kuendelea kuimarisha muungano, kwa kuwa na sera zinazoingiliana pia kuimarisha katiba za pande zote mbili zenye wajibu wa kuboresha maisha ya Watanzania.

"Mfano, uchumi wa buluu unahusisha watumiaji wa bahari wa pande zote, kwa hiyo sera lazima zishirikiane, pia kwenye utalii lazima kuwe na sera zinazofanana."

Jaji Warioba ametilia mkazo kuimarishwa muungano kwa kuwa na umoja, kudumisha amani na haki ya raia popote pale.

Imeandaliwa na Zaituni Mkwama, Frank Buliro na Ismaily Kawambwa.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live