Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wapya, wa zamani kura za maoni CCM wanyukana

B531089432ff1ab6b8cc017a6fb87d69.png Wapya, wa zamani kura za maoni CCM wanyukana

Thu, 23 Jul 2020 Chanzo: habarileo.co.tz

MATOKEO ya kura za maoni kwenye Chama Cha Mapinduzi (CCM) katika majimbo 264 nchini yamekamilika, baadhi ya wabunge na vigogo wameongoza na wengine wameanguka huku mawaziri, wabunge wa zamani na sura mpya wakiendelea kutamba.

Katika mchakato huo ambao hatma ya wagombea itakamilishwa na vikao vya juu vya chama hicho, pia yapo majina ya waliokuwa viongozi katika serikali ya Awamu ya Tano wameanguka.

Mchakato huo wa awamu ya kwanza ulianza Julai 14 na kumalizika rasmi juzi, huku ukiacha doa pia kwa baadhi ya wateule walioingia kwenye kinyang’anyiro hicho na kubwagwa.

Majina makubwa na mawaziri yaliyofanya vyema kwenye kura hizo za maoni ni pamoja na Waziri, Mkuu Kassim Majaliwa aliyepita bila kupingwa katika jimbo la Ruangwa kwa kuwa alikuwa mgombea pekee.

Mawaziri wengine waliongoza kwenye kura hizo ni Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu (Tanga Mjini) na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Profesa Palamagamba Kabudi (Kilosa).

Wengine ni Naibu Waziri wa Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi, Atashasta Nditiye (Muhambwe), Waziri wa Kilimo, Japhet Hasunga (Vwawa), Waziri wa Viwanda na Biashara, Innocent Bashungwa (Karagwe) na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Jenista Mhagama (Peramiho).

Wengine waliong’ara ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Selemani Jafo (Kisarawe), Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi (Isimani), Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Utumishi na Utawala Bora, George Mkuchika (Newala Mjini) na Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Dk Angeline Mabula (Ilemela).

Wengine ni Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa Joyce Ndalichako (Kasulu Mjini) aliyembwaga aliyekuwa Mbunge wa jimbo hilo, Daniel Nsanzugwanko, Waziri wa Madini, Doto Biteko (Bukombe), Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Philip Mpango (Manyovu) na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, George Simbachawene (Kibakwe).

Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara, Stella Manyanya (Nyasa), Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Dk Ashatu Kijaji (Kondoa), Spika wa Bunge la Tanzania Job Ndugai (Kongwa) na Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk Godwin Mollel (Siha) akimbwaga aliyekuwa Mkuu wa Tabora, Aggrey Mwanri.

Mawaziri wengine ni aliyekuwa Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Faustine Ndugulile (Kigamboni) aliyembwaga aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda na Naibu Waziri wa Tawala za mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi) Mwita Waitara (Tarime Vijijini).

Pia, Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk Hamis Kigwangalla aliongoza kwa kura Nzega vijijini. Aidha, wamo wabunge wa kuteuliwa na Rais John Magufuli waliong’ara katika kura hizo za maoni ambao pamoja na Profesa Kabudi ni Naibu Spika wa Bunge, Dk Tulia Ackson (Mbeya Mjini), Salma Kikwete (Mchinga), na Anne Kilango Same (Mashariki).

Katika kinyang’anyiro hicho zipo sura mpya zilizoibuka na ushindi kwenye kura hizo za maoni ikiwa nyingine ni mara ya kwanza kujitokeza na nyingine zilishawahi kuwania awali na kukosa.

Sura hizo mpya ni Kirumbe Ngenda (Kigoma Mjini), Shaaban Shekilindi (Tanga), Noel Severe (Arumeru Magharibi) aliyembwaga aliyekuwa Mbunge wa jimbo hilo Goodluck Ole Medeye, Furaha Jacob (Kawe), Jerry Slaa (Ukonga), Issa Mtemvu (Kibamba), Nawanda Yahaya (Newala), Ally Makoa (Kondoa Mji) na Moses Kaegele (Nkasi Kusini) aliyembwaga aliyekuwa Mbunge wa jimbo hilo Deusderius Mipata.

Aidha, wanachama wengine walioshinda kura za maoni kwa mara ya kwanza ni Method Kamamba aliyembwaga aliyekuwa Mbunge wa jimbo hilo Christopher Chiza (Muhambwe), Abubakari Assenga (Kilombero), Dk Grasmus Sebuyoya (Biharamulo) na Almasoud Kalumuna (Bukoba Mjini).

Wengine walioongoza ni Aden Mwakyonde (Tunduma), Wilman Ndile (Ileje) aliyembwaga aliyekuwa mbunge wa jimbo hilo Janet Mbene, George Mwenisongole (mbozi), Innocent Bilakwate (Kyerwa), Amos Makalla (Mvomero) akimbwaga aliyekuwa Mbunge wa jimbo hilo Selemani Sadiq na Charles Sungura (Handeni Vijijini) akimbwaga aliyekuwa Mbunge, Mboni Mhita.

Pia wamo Deus Sangu (Kwela), Enock Koola (Vunjo) aliyembwaga aliyewahi kuwa Mkurugenzi Mtendaji Benki ya CRBD, Dk. Charles Kimei na Abbas Tarimba (Kinondoni) aliyembwaga aliyekuwa Mbunge wa jimbo hilo Idd Azan na Ally Makoa (Kondoa Mjini) akimbwaga aliyekuwa Mbunge wa jimbo hilo Edwin Sanda.

Aidha, wengine ni Antipas Mngungus (Malinyi) akimbwaga aliyekuwa Mbunge wa jimbo hilo Dk Hadji Mponda, Hamis TaleTale (Morogoro Kusini Mashariki) akimbwaga aliyekuwa Mbunge wa jimbo hilo na Naibu Waziri wa Kilimo, Omary Mgumba, Reuben Kwagirwa (Handeni Mjini) na Masunga Biteko (Busanda).

Sura nyingine mpya ni Yahya Mhata (Nanyumbu), Omar Kigua (Kilindi) aliyembwaga mwanasiasa mkongwe Dk Aisha Kigoda, Jackson Ryoba (Tarime Mjini), Oran Njeza (Mbeya Vijijini) na Masache Kasaka (Chunya) aliyembwaga aliyekuwa Mbunge wa jimbo hilo Victor Mwambalaswa.

Wengine ni Saul Amon (Rungwe), Ally Mlagila (Kyela) aliyempita kwa kura Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk Harrison Mwakyembe aliyekuwa Mbunge wa jimbo hilo na Salim Hasham (Ulanga) akimpita kwa kura aliyekuwa Mbunge wa jimbo hilo, Goodluck Mlinga.

Jonas Nkya aliongoza katika kura hizo za maoni katika jimbo la Mikumi, Gordwin Emmanuel pamoja na Rose Rwakatare walifungana kwa kura jimbo la Mlimba, Muharami Mkenge (Bagamoyo) aliyembwaga aliyekuwa Mbunge wa jimbo hilo Shukuru Kawambwa na Omary Kipanga (Mafia) aliyembwaga aliyekuwa Mbunge wa jimbo hilo Mbaraka Dau.

Sura nyingine mpya kwenye kinyang’anyiro hicho Twaha Mpembenue (Kibiti), Ndaigaaba Ruhoro (Ngara) akimbwaga aliyekuwa Mbunge wa jimbo hilo Rafael Gashaza na Henry Kabeho (Igunga) akimbwaga aliyekuwa Mbunge wa jimbo hilo Dk Dalaly Kafumu.

Aidha, Venant Protas aliongoza kura za maoni jimbo la Igagula akimbwaga mwanasiasa mkongwe na aliyewahi kuwa Naibu Waziri wa Uchukuzi awamu ya Tatu Dkt Athumani Mfutakamba, Seif Gulamali (Manonga), Shafin Sumar (Tabora Kaskazini) na Rehema Magila (Ulyankulu) Katika kinyang’anyiro hicho aliyekuwa Katibu Mkuu Wizara ya Maji, Profesa Kitila Mkumbo ameongoza Ubungo, Mrisho Gambo (Arusha), aliyekuwa Mkurugenzi wa Mtendaji Wagombea Ubunge Jimbo la Kawe kwa tiketi ya CCM wakihakiki kura zao kabla ya kutangazwa mshindi wa kura za maoni kwenye mkutano uliofanyika Mbezi Beach, Dar es Salaam juzi.

Katika uchaguzi huo, Furaha Jacob (wa tatu kushoto mwenye kofia) aliongoza kwa kupata kura 101 na kufuatiwa na Angela Kiziga kwa kura 85. (Picha na Fadhili Akida). wa Halmashauri ya Wilaya ya Mvomero mkoani Morogoro, Frolent Kyombo (Nkenge) na kumpita aliyekuwa Mbunge wa jimbo hilo, Balozi Dk Diodorus Kamala. Mtendaji mwingine wa serikali aliyeongoza katika kura hizo ni aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Njombe Christopher Ole Sendeka (Simanjiro), aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Kongwa, Deo Ndejembi (Chilonwa) akimbwaga aliyekuwa Mbunge wa jimbo hilo, Joel Mwaka.

Wabunge walioongoza kwenye kura za maoni ni Peter Serukamba (Kigoma Kaskazini), Augustino Vuma (Kasulu Vijijini), Ahmed Shabiby (Gairo), Hawa Ghasia (Mtwara Vijijini), Livingstone Lusinde (Mtera), Nape Nnauye (Mtama), Prudenciana Kikwembe (Kavuu), Moshi Kakoso (Mpanda Vijijini) na Sebastian Kapufi (Mpanda Mjini).

Wengine ni Anna Lupembe (Nsimbo) aliyembwaga aliyekuwa Mbunge wa jimbo hilo Richard Mbogo, Josephat Kandege (Kalambo) aliyembwaga aliyewahi kuwa Naibu Waziri wa Elimu na pia Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Ludovick Mwananzila.

Pia aliyeongoza kwenye kura hizo ni Aeshi Hilaly (Sumbawanga), George Lubeleje (Mpwapwa), Mussa Hassan ‘Zungu’ (Ilala) aliyembwaga aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Ilala Sophia Mjema, January Makamba (Bumbuli), Ridhiwani Kikwete (Chalinze) na David Mathayo (Same (Magharibi) akimbwaga aliyekuwa Waziri wa Uwekezaji Angella Kairuki.

Wabunge wengine waliongoza ni Hasna Mwilima (Kigoma Kusini), Charles Mwijage (Muleba Kaskazini), Jumaa Aweso (Pangani). Wengine ni Dk Stephen Kiruswa (Longido), Hamida Abdallah (Lindi)na William Ole Nasha (Ngorongoro), Joseph Mhagama (Madaba) akimbwaga aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Tarime, Glorius Luoga.

Wengine ni Adadi Rajabu (Muheza), Abdallah Chikota (Nanyamba), Silvestry Koka (Kibaha Mjini), Margaret Sitta (Urambo), Selamani Zedi (Bukene), George Kakunda (Sikonge) Aidha, wamo wabunge na watendaji waliohamia CCM wakiunga mkono juhudi za Rais Magufuli kutoka vyama vya siasa ambao kwenye matokeo hayo wameanguka akiwemo aliyekuwa Katibu Tawala Songwe, David Kafulila (Kigoma Kusini) na aliyekuwa Mbunge wa Momba (Chadema), David Silinde na Silinde alikuwa anawania ubunge Jimbo la Tunduma. Wengine ni Maulid Mtulia (Kinondoni), Peter Lijualikali (Kilombero), Abdallah Mtolea, (Temeke), Joshua Nassari (Arumeru Mashariki), Dk Vicent Mashinji (Kawe).

Bado mchakato wa kuchuja majina hayo yaliyoongoza ngazi za juu unaendelea ambapo kwa mujibu wa ratiba ya CCM hadi katikati ya Agosti, Kamati Kuu ya chama hicho itaweka bayana mgombea katika kila jimbo.

Chanzo: habarileo.co.tz