Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wapinzani wamuita msajili kujadili uchaguzi wa serikali za mitaa

82891 Pic+vyama Wapinzani wamuita msajili kujadili uchaguzi wa serikali za mitaa

Tue, 5 Nov 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Vyama vya upinzani nchini vimemuomba Msajili wa Vyama vya Siasa, Jaji Francis Mutungi na mwenyekiti wa baraza la vyama hivyo John Shibuda kuitisha kikao cha vyama vya siasa ili kujadili changamoto zilizojitokeza kwenye mchakato wa uchaguzi wa Serikali za Mitaa.

Vyama hivyo ni Chadema, CUF na ACT-Wazalendo kwa nyakati tofauti vimekuwa vikitoa malalamiko kuhusu changamoto na kile walichodai kuwa ni hujuma wanazofanyiwa wagombea wa vyama vya upinzani kwenye uchaguzi huo.

Kutokana na changamoto hizo kukithiri ikiwemo wagombea kunyimwa fomu na ofisi kufungwa, viongozi wa vyama hivyo walikwenda mbali kwa kumuomba Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Tamisemi), Seleman Jafo kuingilia kati changamoto hiyo.

Akizungumza leo Jumatatu Novemba 4, 2019 kwa niaba ya viongozi wenzake wa vyama vya CCK, UDP, ADC, TLP, NRA, Demokrasia  Makini, Sau, AFP, Tadea katibu mkuu wa DP, Abdul Mluya amesema wana imana kikao hicho kitatibu makovu hayo.

"Tunataka tupate ufumbuzi wa matatizo yote yaliyojitokeza na baraza ndio chombo pekee kitakachotusaidia kuondoa sintofahamu hii.Tutajadiliana na kupata muafaka na tiba kuhusu hali hii.

"Kwa kuwa nchi yetu ina miongozo na sheria, sisi tumeamua twende na njia hii badala ya kulalamika kwenye mitandao ya kijamii.Tunamuomba msajili afanye haraka kuitisha kikao hiki akizingatia leo ni siku ya uteuzi," amesema Mluya. Mluya amesema changamoto waliozibaini na kutaka kujadili katika kikao hicho ni pamoja na ofisi kufungwa na wagombea wa upinzani kunyimwa fomu huku akimtaka Jaji Mutungi kuharakisha mchakato huo kabla ya kampeni za uchaguzi huo kuanza.

Chanzo: mwananchi.co.tz