Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wapinzani waibuka na makinikia bungeni

60003 Pic+wapinzani

Tue, 28 May 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dodoma. Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni imehoji kwa nini Kampuni ya Accacia bado inaendelea na shughuli za uchimbaji wa madini nchini wakati Taifa liliambiwa kuwa ni wezi wa rasilimali za nchi.

Kauli hiyo imetolewa leo Mei 27, 2019 na msemaji mkuu wa wizara hiyo, John Heche alipokuwa akiwasilisha maoni ya kambi hiyo kuhusu makadirio ya mapato na matumizi ya Wizara ya Madini kwa mwaka 2019/2020.

“Na ikiwa Serikali iliwadanganya Watanzania ni lini sasa Serikali itajitokeza hadharani kufafanua jambo hili lililogubikwa na sintofahamu wakati Watanzania wakiendelea kusubiri magari ya Noah nchi nzima kama ilivyoahidiwa na Serikali?” Amehoji.

Amesema kamati ya makinikia iliainisha aina nyingine za madini kwenye nyaraka za usafirishaji wa makontena yaliyokamatwa bandarini ikiwa ni pamoja na sulphur, chuma na madini ya mkakati yaani Iridium, Rhodium, Ytterbium, Berylium, Tantalum na Lithium.

Hata hivyo, amesema mpaka sasa Serikali inazungumzia madini ya dhahabu, fedha na shaba pekee.

Chanzo: mwananchi.co.tz