Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wapiga kura wachache wajitokeza Hai

Mon, 17 Sep 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Hai. Uchaguzi mdogo wa marudio katika kata mbili za wilaya ya Hai mkoani Kilimanjaro unaendelea huku idadi ya wananchi waliojitokeza kupiga kura hadi kufikia saa 5 asubuhi leo Jumapili Septemba 16, 2018 ikiwa ndogo.

MCL Digital leo imefika katika vituo vya kupigia kura katika kata hizo za Machame Uroki na Kia na kushuhudia idadi ndogo ya wapiga kura, huku mawakala na wasimamizi wakiwa wameketi wakisubiri watakaojitokeza.

Kata ya Machame Uroki, MCL Digital imepita katika vituo vya Shule ya Msingi Uraa, Ufumbo na Uswaa na kata ya Kia katika vituo vya  Sanya Stesheni, Mtakuja, Zahanati na Tindigani.

Baadhi ya wasimamizi wa vituo hivyo kwa sharti la kutotajwa majina wamesema huenda wananchi wengi watajitokeza muda wa mchana baada ya kutoka kanisani.

Ofisa uchaguzi wilaya ya Hai, Rajab Yateri amesema mpaka sasa hali ni shwari katika vituo vyote, ana imani uchaguzi huo utafanyika kwa amani na utulivu.

Chanzo: mwananchi.co.tz