Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wanawake washikana ‘uchawi’ kwenye chaguzi

Tue, 18 Jun 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Morogoro. Wanawake wametajwa kuwa moja ya kundi lililo nyuma katika kugombea uongozi kwa nafasi za kuchaguliwa tofauti na wanaume huku baadhi ya sababu zikitajwa ni wenyewe kwa wenyewe kushindwa kusaidiana pale mmoja wao anapojitokeza.

Hayo yamesemwa Jumatatu Juni 17, 2019 wakati wa mafunzo ya elimu ya jinsia, demokrasia na uongozi yaliyoandaliwa na Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP) kwa viongozi wa taasisi mbalimbali zisizo za kiserikali, taasisi za serikali ngazi ya kata na viongozi wa madhehebu ya dini ngazi ya kata mkoani Morogoro.

Akizungumza wakati wa mafunzo hayo, mmoja wa washirika, Juma Ngwalu alisema changamoto wanayopata wanawake wanaogombea nafasi mbalimbali katika uchaguzi, adui mkubwa ni mwanamke mwenyewe.

Ngwalu alisema baadhi ya wanawake hawapendi wakiona mwenzao wanashinda uchaguzi mbele ya wanaume kwa madai wanapopata nafasi wamekuwa wakilinga na kuonyesha majivuno.

“Wanawake wanachukiana wenyewe kwa wenyewe hasa mmoja wao anapojitokeza kugombea nafasi amekuwa akipingwa kwanza pale anapotoka iwe kwenye chama ama kijiji hiyo ni moja ya sababu inayowakwamishwa baadhi yao kuingia kwenye uongozi wa kupigiwa kura tofauti na wanaume,” alisema Ngwala.

Kwa upande wa Tatu Maleta mshiriki wa mafunzo hayo alisema kuwajengea uwezo wa kujua jinsi na jinsia katika demokrasi ni moja ya njia ya kuwasaidia hasa wanaporudi vijijini watawahamasisha wanawake, vijana na makundi ya watu wenye ulemavu kuingia kwenye uongozi kwa nafasi za kugombea.

Pia Soma

“Mwanamke anaposimama haungwi mkono na wanaume lakini na wanawake hapo ndipo tunakosa nafasi kwenye uongozi na sababu nyingine wanawake hatupendani na ukiangalia kama tukiunganisha nguvu ya pamoja tunaweza,” alisema Tatu.

Chanzo: mwananchi.co.tz