WANAWAKE waliofanikiwa katika nyanya za kisiasa, kiuchumi, kielimu na kijamii wametakiwa kuonesha njia kwa wasichana wanaochipukia katika uongozi na siasa ili baadaye kuwa viongozi bora.
Kauli hiyo ilitolewa na Kaimu Katibu wa Jumuiya ya Umoja wa Wanawake wa CCM (UWT) Wilaya ya Mpwapwa, mkoani Dodoma, Savera Simbachawene katika mahojiano na HabariLEO.
Savera alisema wapo wanawake walioweza kuonesha mwanga na mafanikio makubwa katika taifa hili kwa nyanja za kiongozi, kisiasa , kielimu na kijamii na kuweza kuisadia jamii katatua changamoto zinazowakabili.
Aidha alisema serikali imetambua jitihada na thamani ya mwanamke na kumuwekea mazingira rafiki ya kushiriki katika nafasi mbalimabli za uamuzi.
Alisema pamoja na serikali kuweka mazingira rafiki kwa wanawake lakina bado kuna changamoto zinamkabili mwanamke na mtoto wa kike.
Alisema serikali inatambua changamoto anazopitia mtoto wa kike na mwanamke na kuziwekea sera miongozo pamoja na mikataba mbalimbali ya kikanda na kitaifa ya kupinga unyanyasaji na ukatili wa kinjisia ili kuweza kufikia usawa wa kijinsia.
Kwa upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Mwanamke na Mafanikio, Maria Mapunda alisema shirika tangu lipate usajili limejikita katika kumjengea uwezo mtoto wa kike ilioko shuleni kujitambua, kujiamini na kudhubutu bila kuangalia changamoto zinazowakabili.
Mmoja wa wakazi wa Mpwapwa, Modesta Makalanga alisema ili wanawake waweze kufanikiwa lazima waongeze nidhamu katika kile wanachokifanya na kuwatii viongozi waliowatangulia.