Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wanawake tembeeni kifua mbele CCM ipo imara-Naibu Katibu Mkuu

Wanawake Tembeeni Kifua Mbele CCM Ipo Imara Naibu Katibu Mkuu CCM Wanawake tembeeni kifua mbele CCM ipo imara-Naibu Katibu Mkuu

Thu, 17 Nov 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Naibu Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Tanzania Bara, Christine amewataka Wanawake wote nchini kutembea kifua mbele kwani Chama cha Mapinduzi CCM kipo imara.

Hayo ameyasema leo Novemba 17,2022 jijini Dodoma wakati akifungua Mkutano Mkuu wa Uchaguzi wa Umoja wa wanawake Tanzania (UWT),Mkoa wa Dodoma.

Bi.Mndeme amewataka wagommbea wa nafasi mbalimbali kuzingatia mambo matano ikiwa ni pamoja na kwenda kusimamia uhai wa chama.

"Nawaomba Wanawake ppopote mlipo mtembee kifua mbele Chama kipo imara tena zaidi ya sana hivyo tuendelee kusimamia ilani ya chama chetu”amesema.

Ametaja mambo mengine ya kuzingatia nia pamoja na kuzingatia ratiba ya vikao vya kikanuni,kusimamia suala la kuongeza wanachama wapya,kujisajili kwa mfumo wa kieletroniki na kusimamia ulipaji wa ada.

Aidha amewataka wagombea watakaochaguliwa kwenda kusimamia iIani ya CCM pamoja na kunena mazuri ya ya Mwenyekiti wa CCM na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Samia Suluhu Hassan.

Kwa upande wake, Katibu Mkuu wa UWT Dkt.Philis Nyimbi amewaasa wanawake kuendelea kuunga mkono juhudi za Rais Samia Suluhu Hassan za kuwaletea watanzania maendeleo.

Awali,Mwenyekiti wa UWT Mkoa wa Dodoma anayemaliza muda wake, Neema Majule amesema kama Jumuiya katika kipindi cha miaka mitano wameweza kufanya siasa na uchumi kwa kuanzisha shule ya chekechekea na kujenga fremu za maduka.

Mkutano huo unawashirikisha wajumbe 536 ambapo jumla ya wanachama wanne wamepitishwa kugombea nafasi hiyo ambao ni Neema Majule, Kaundime Kasase, Elizabeth Lameck na Zabibu Mafta.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live