Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wanawake CCM watwishwa zigo

46203 Pic+wanawake Wanawake CCM watwishwa zigo

Tue, 12 Mar 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Pemba. Tangu uchaguzi mkuu wa kwanza ulioshirikisha vyama vingi mwaka 1995, CCM haijawahi kushinda kiti cha ubunge au uwakilishi kisiwani hapa mpaka CUF iwe imesusia.

Kwa sasa wanawake Pemba wametakiwa kujipanga kwa umakini uchaguzi mkuu wa mwakani kuhakikisha wanaipa CCM ushindi mkubwa.

Hayo yalisemwa na mwenyekiti wa Jumuiya ya Wanawake wa CCM Tanzania (UWT) Gaudencia Kabaka, alipozungumza na wanawake mkoa wa Kusini Pemba.

Kabaka alisema wanawake wana mchango mkubwa kwa chama ndiyo wanaokutana na makundi mengi ya watu hivyo watumie fursa hiyo kuwashawishi wengine kujiunga nao ili kuongeza idadi ya wapiga kura.

Awali katibu mkuu wa UWT Queen Mlozi, aliwataka wanawake hao kujipanga kimalezi ili watoto wao wakike wasikatishe masomo kwa sababu ya ndoa.

Mlozi alisema mtoto wa kike anatakiwa apitie hatua nne ikiwamo elimu ya msingi, sekondari, chuo kikuu, ndoa kisha kubeba ujauzito akiwa ndani ya ndoa yake.

Naye makamu mwenyekiti wa UWT Zanzibar, Thuwaiba Kisasi, alisema nguvu ya chama ni jumuiya zake ikiwamo UWT hivyo kila mmoja ana wajibu wa kusimamia uhai wa CCM.

Mwenyekiti wa UWT mkoa wa Kusini Pemba, Bimkuba Khamis Mohamed, alisema hali ya kisiasa katika mkoa wake ni nzuri, kila mwananchi anaendelea na shughuli zake za maendeleo.



Chanzo: mwananchi.co.tz