Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wanawake ACT Wazalendo wahamasishwa kuwania uongozi

ACT.jpeg Wanawake ACT Wazalendo wahamasishwa kuwania uongozi

Thu, 1 Feb 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Zikiwa zimebaki siku kadhaa chama cha ACT-Wazalendo kufanya mkutano wake mkuu, mjumbe wa kikosi kazi ngome ya wanawake, Halima Ibrahim amewataka wanawake wa chama hicho kujitokeza kwa wingi kuwania nafasi za uongozi.

Amesema hayo leo Februari mosi, 2024 alipozungumza na viongozi wa mikoa wa saba ya kichama kwa upande wa Unguja na kueleza wakati umefika kwa wanachama hao kutobaki nyuma.

Amesema kujitokeza kwa wingi wanawake kwenye uchaguzi huo kutatoa fursa nyingi zaidi kwao kuingia kwenye nafasi za uamuzi ndani ya chama ambazo ni muhimu.

Amewataka kuacha kuendelea na dhana kuwa wanawake ni watu wanaopaswa kugombea kwenye ngome yao pekea, badala yake wajitokeze hata kuwania nafasi ya hata ya Mwenyekiti Taifa.

“Chama hiki ni chetu sote, hakuna mwenye hatimiliki. Sote ni sawa, ninachowataka twendeni tukagomee tushike nafasi muda umefika,” amesema.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa kikosi kazi Ngome ya Wanawake, Pavu Abdalla amesema wanawake wanapoingia kwenye nafasi za uongozi wa chama inakua rahisi kufikisha ajenda zao kwenye ngazi ya Taifa.

Amesema kwa miaka mingi wanawake wa vyama vya siasa wamekuwa nyuma kushiriki kwenye nafasi muhimu za uamuzi katika vyama vyao.

Akizungumza na Mwananchi Digital baada ya mkutano huo, ofisa mradi wa kuwawezesha wanawake kushika nafasi za uongozi kutoka Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake Tanzania (Tamwa) Zanzibar, Maryam Ame amesema wanawake zaidi ya 600 wamejengewa uwezo na wapo tayari kujitokeza muda utakapofika.

“Sisi tunaamini kuwa Zanzibar itabadilika baada ya uchaguzi wa 2025, wanawake wengi zaidi wataingia kwenye vyombo vya kutunga sheria katika Baraza la Wawakilishi na Bunge,” amesema.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live