Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wanasiasa wasiibeze Serikali tatizo la maji-Mwenyekiti CCM

IMG 20221031 WA0045 Wanasiasa wasiibeze Serikali tatizo la maji-Mwenyekiti CCM

Tue, 1 Nov 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Bagamoyo, Abdulsharifu Zahoro amewaasa baadhi ya wanasiasa na wananchi wanaoikashifu na kudai Serikali inakwama kutokana na ukame na changamoto ya upungufu wa maji, wasitafute umaarufu, waache propaganda na badala yake wajenge tabia ya kuwa kitu kimoja kwenye masuala yanayogusa Taifa.

Aidha amesema, ipo haja kwa Serikali kuangalia namna ya kuingiza vyanzo vya maji (Ruvu na WAMI) kwenye hifadhi za Taifa, hatua itakayosaidia kuimarisha ulinzi ili kulinda vyanzo hivyo.

Sharifu alitoa rai hiyo ,wakati alipokutana na Waandishi wa Habari Bagamoyo, na kuulizwa utekelezaji wa ilani na usimamizi wa Serikali kwenye upande wa huduma ya maji, ili kutatua kero ya mgao wa maji .

Alisema Serikali imefanya makubwa katika sekta ya maji ,kusambaza maji nchini pamoja na wilaya ya Bagamoyo kwasasa tatizo limepungua kwa kiasi kikubwa kutokana na utekelezaji wa miradi mikubwa ya maji, Ila changamoto zinajitokeza kutokana na uharibifu mkubwa wa vyanzo vya maji ikiwemo WAMI.

Alieleza, wanaogeuza changamoto ya maji kukashifu Serikali ,hawana jipya kwani wananchi wanaona jitihada zinazofanywa na Serikali kutatua kero mbalimbali .

Hata hivyo alishauri, vyanzo vya maji vikiingizwa kwenye hifadhi za Taifa itapunguza adha ya uhaba wa maji na kuongeza ulinzi katika vyanzo hivyo.

"Kuna mabadiliko ya tabia ya nchi, lakini pia tuiombe Serikali ione umuhimu wa kuviingiza vyanzo hivyo kwenye hifadhi za Taifa, itatusaidia maana kwasasa wapo wanaoenda kulima karibu na maeneo hayo, wengine wanaingiza mifugo bila kudhibitiwa."

Sharif alifafanua, hali ya mgawo wa maji kipindi cha kiangazi itaendelea kutukumba kipindi cha kiangazi" endapo baadhi ya watu wakiwa hawatunzi vyanzo vya maji.

Mwenyekiti huyo aliipongeza Serikali kwa jitihada ambazo inaendelea kufanya kukabiliana na uhaba wa maji, ambapo pia alisema katika Wilaya yake wanatarajia kufanya maombi kwa ajili ya kuiombea mvua.

Vilevile alimpongeza Rais Samia Suluhu Hassan kwa fedha anazoendelea kutoa kukamilisha miradi ya kimkakati ikiwemo daraja la Wami, Mlandizi-Chalinze-Mboga ambayo ipo mengine inayotekelezwa na DAWASA na mingine inatekelezwa na RUWASA.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live