Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wanasiasa vijana wampongeza Rais Samia

Wanasiasa Vijana Wampongeza Rais Samia.jpeg Wanasiasa vijana wampongeza Rais Samia

Tue, 11 Apr 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Wanasiasa Vijana Tanzania (WAVITA) wamempongeza Rais Samia Suluhu Hassan kwa hatua anazoendelea kuzichukua dhidi ya viongozi wabadhirifu Nchini.

Akizungumza Jijini Dar es Salaam jana Mwenyekiti wa WAVITA George Shiganga, alisema kazi anayofanya Rais ni kubwa lakini wapo baadhi ya viongozi wanamvunja moyo kwenye utendaji.

Alisema wao kama vijana wanampongeza na kumuunga mkono na pia wako bega kwa bega na yeye kuhakikisha watanzania wanapata mafanikio makubwa.

"Sisi kama WAVITA tunaendelea kumpongeza Rais kwa hatua anazozichukua kwa viongozi wasiokuwa waaminifu kwani anakopa fedha kwa ajili yetu lakini viongozi hawamtendei haki kwa kutumia fedha vibaya'; alisema Mwenyekiti huyo.

Aidha, alisema kuwa niwakati muhafaka kwa vijana Nchi mzima kutoka na kuungana kumuunga mkono Rais kwa kukataa rushwa, kukataa rushwa pamoja na wabadhirifu.

Hata hivyo alisema kuwa kazi ya Rais inaonekana kutokana na kwamba anachukua hatua kwa wale wanaokiuka maagizo lakini pia miundombinu iko vizuri ikiwemo upatikanaji wa maji safi na salama.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live