Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wanaosubiri mpasuko Chadema watasubiri sana - Mbowe

Mbowe Db Wanaosubiri mpasuko Chadema watasubiri sana - Mbowe

Sun, 14 Jan 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Taifa, Freeman Mbowe, amesema wanaotegemea chama hicho kipasuke kutokana na migogoro watasubiri sana. 

Akizungumza na waandishi wa habari leo tarehe 13 Januari 2024, jijini Dar es Salaam, Mbowe amesema mpasuko ndani ya Chadema haupo na kwamba kilichopo ni baadhi ya watu kutofautiana mtazamo kitu alichokiita kuwa ni afya kwa demokrasia.

“Na wale wanaofikiri kuwa chama hiki kina mgogoro watasubiri sana, wote ambao wanafikiri kuna mpasuko Chadema haupo na hautakuwepo. Tutakilinda na kukihami chama hiki kwa gharama yoyote umoja wetu ni muhimu kuliko mtu yoyote,” amesema Mbowe.

Mbowe amesema “chama cha siasa ni kisima cha fikra na asitokee binadamu yoyote akafikiri kwa kuwa kwenye chama kimoja wote mtafikiri mamoja, hiyo ni kinyume na asili ya binadamu hata kwenye familia yako mnatofautiana katika masuala lakini mkiitofautiana ni afya hivyo sioni mnaonaje kuwa na viongozi na mawazo tofauti yanayokinzana eti ni mgogoro, sio mgogoro.”

Akizungumzia kuhusu Chadema kujitoa kwenye maridhiano na Chama Cha Mapinduzi (CCM), Mbowe amesema uamuzi huo unatokana na chama chake kukosa imani dhidi yake kufuatia hatua ya Serikali iliyoko madarakani kupeleka miswada ya marekebisho ya sheria za uchaguzi ambayo haijabeba maoni yao.

“Huyu mama (Rais Samia), tumekaa naye vikao  ningestahili kumuamini lakini leo nasema simuamini sababu chama chake kimepeleka miswada ambayo haiakisi zile R zake nne anazohubiri yeye na wenzake. Kiongozi unapaswa kutembea kwenye maneno yako unayotoa,” amesema Mbowe.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live