Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wanaohama wanatoa fursa kuwajua-Mwalimu

10523 Pic+mwalimu TanzaniaWeb

Tue, 7 Aug 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Tanga. Naibu Katibu Mkuu wa Chadema (Zanzibar), Salum Mwalimu amesema hatua ya wabunge na madiwani wa vyama vilivyo chini ya Ukawa kujiuzulu na kuhamia CCM kunatoa nafasi ya kuwatambua wanachama na viongozi wasio na nia ya dhati ya kuwaletea wananchi mabadiliko kidemokrasia.

Mwalimu amesema hali hiyo haiwezi kuwayumbisha viongozi wa vyama hivyo badala yake watapambana hadi kuhakikisha Watanzania wanakuwa na uhuru wa kuzungumza na kuwachagua viongozi wanaowataka.

Alisema hayo juzi katika mkutano wa kampeni ya kumnadi mgombea wa udiwani wa Kata ya Makorora Jijini Tanga, Zainab Ashraf uliofanyika katika uwanja wa Sokoni mjini hapa.

Mwalimu alisema kuikosoa, kuishauri na kufichua matendo mabaya ya serikali ndiyo wajibu wao kama wapinzani, hivyo wataendelea na kazi hiyo ili kujenga uwajibikaji na uadilifu.

Kiongozi huyo alisema kitendo cha wanasiasa kukubali kufungwa midomo ni sawa na muumini kuacha kufanya ibada na kutumikia dhambi pasipo sababu za msingi.

Aliwataka wananchi kutosikiliza propaganda za kisiasa kuhusu uchumi na maendeleo yao kwa ujumla kwa kuwa kila mmoja anaona hali ya maisha (Burhani Yakub).

Chanzo: mwananchi.co.tz