Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

"Wananchi hawajadi Katiba, ni hitaji la kisiasa" - Katibu Mkuu CCM

CHONGOLO12.jpeg Daniel Chongolo, Katibu Mkuu Chama Cha Mapinduzi Taifa (CCM )

Wed, 11 Aug 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi CCM, Godfrey Chongolo, amejibu hoja za wanasiasa wa vyama vya Upinzani kuhusu madai ya katiba mpya, kwa kusema kuwa maadai hayo sio haka ya wananchi bali kwa aajili wanasiasa.

chongolo ameyasema hayo leo Agost 11 mwaka huu, wakati wa mkutan wake na Waandishi wa habari, na kubainisha kuwa wanachi hawajawahi kudai katiba.

"Wapi uliona wananchi wamedai katiba mpya, dai la katiba mpya ni letu sisi wanasiasa, hivi kupitia kupatikana kwa katiba mpya itawaletea wananchi unga? Katiba mpya inayodaiwa na wanasiasa ni kwa ajili ya kutengeneza nafasi za uongozi na madaraka."

aliongeza kusema kuwa mambo yanayodaiwa kwenye katiba mpya ni machache sana, huku akisistiza juu ya hoja ya uhuru wa kisiasa kuwa upo wa kutosha tofauti na wapinzani wanavyodai.

"Mambo yanayodaiwa kwenye katiba mpya na wanasiasa ni machache sana, kwanza ni Tume Huru, pili ni uhuru wa kisiasa na demokrasia, hivi Tanzania haina uhuru? Ukitembelea nchi ambazo hazina uhuru utajua Tanzania tuna uhuru wa demokrasia." -Daniel Chongolo, Katibu Mkuu wa CCM.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live