Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wanachama watofautiana kuhusu uamuzi wa Lembeli kurudi CCM

9632 Pic+wanachama

Thu, 21 Jun 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Kahama. Siku chache baada ya James Lembeli kutangaza kurudi CCM, kumetokea kutoelewana baina ya Umoja wa Wazee Wilaya ya Kahama na Katibu wa Siasa na Uenezi wa CCM, Kahama, Joachim Simbila.

Juni 13, Lembeli alitangaza kurudi CCM akitokea Chadema alikojiunga mwaka 2015.

Lakini baada ya kutangaza kurudi kwake, Simbila alionekana kupinga kurudi kwa Lembeli, akisema hakufuata taratibu.

Simbila pia alitumia mitandao ya kijamii kupinga uamuzi wa Lembeli.

Katibu wa Umoja wa Wazee Wilaya ya Kahama (Uwaka), Paulo Ntelya alisema Lembeli amefanya uamuzi wa kurudi CCM na kama kulikuwa na kasoro Simbila alipaswa kumfuata binafsi na kumpa maelekezo badala ya kusambaza kwenye mitandao.

Ntelya alidai Lembeli yuko sahihi kwani hata wanasiasa wengine hurudi CCM lakini hakuna anayepinga.

“Lembeli ni mwanasiasa wa kitaifa hivyo kupingwa ngazi ya wilaya ni sawa na kukidhalilisha chama, pia CCM inapaswa kuwa mshauri na si mpingaji,” alisema

Simbila alipoulizwa kuhusu jambo hilo alisema Lembeli alipaswa kuandika barua ya kuomba kurudi CCM kabla ya kutangaza kurudi na ndio utaratibu huo unaotambulika

Alipotakiwa kuzungumzia tofauti hizo, Lembeli alisema kwamba hawezi kupingana huku akimtahadharisha Simbila kuacha kutumiwa na wanasiasa kumdhalilisha badala yake afanye kazi yake ya kiutendaji.

Chanzo: mwananchi.co.tz