Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wana CCM 128,000 wajitokea uchaguzi Mara

Wanaccmpic Data Wana CCM 128,000 wajitokea uchaguzi Mara

Sat, 23 Apr 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Jumla ya wanachama 128,757 wa CCM mkoani Mara wamejitokeza kugombea nafasi mbalimbali ndani ya chama hicho kwa ngazi ya shina mkoani humo.

Katibu wa CCM mkoa wa Mara, Lengael Akyoo amewaambia waandishi wa habari mjini hapa kuwa kati ya watu hao, wanachama 19,589 ambao kati yao wanawake wakiwa ni 7,853 wanagombea nafas iya uenyekiti wa shina (balozi) katika uchaguzi amabo unaendelea hivi sasa.

Ameongeza kuwa katika nafasi ya ukatibu jumla ya wanachama 21,225 wamejaza fomu kugombea nafasi hiyo huku kwa nafasi tatu za wajumbe wa shina wakijitokeza wanachama 28,754.

"Katika nafasi za jumuiya za chama jumla ya wanachama 20,713 wamejitokeza kugombea nafasi ya uenyekiti ambapo wanawake wanaogombea nafasi hiyo ngazi ya shina ni 7,853," amesema Akyoo.

Ameongeza kuwa kwa upande wa umoja wa wanawake jumla ya wanachama 18,302 wamechukua fomu huku kwa upande wa wazazi wakijitokeza wanachama 20,174 ambapo kati yao wanawake wakiwa ni 7,102.

Kuhusu mchakato wa upigaji kura katibu huyo amesema kuwa hadi sasa hakuna dosari iliyojitokeza na kwamba tayari upigaji kura kwenye mashina 5,870 umekamilika kati ya mashina 11,246 yaliyopo mkoani Mara.

Advertisement "Hadi sasa tumefika asilimia 52.2 ya upigaji kura kwenye mashina yetu na tunaamini hadi kufika Aprili 30 tutakuwa tumemaliza mchakato huu kwa ngazi ya mashina " amesema.

Akyoo amesema kuwa kujitokeza kwa wingi kwa wanachama kugombea nafsi za uongozi wa chama hicho kwa ngazi ya shina ambapo hakuna malipo ni ishara kuwa wananchi bado wana imani kubwa na chama.

Amefafanua kuwa ili kuhakikisha kuwa chama hicho kinapata ushindi katika chaguzi zijazo za serikali za mitaa na uchaguzi mkuu viongozi watakaochaguliwa kukiongoza chama hicho lazima wawe ni wale wanaokubalika ndani na nje ya chama.

Amesema kuwa mchakato wa uchaguzi wa chama hicho katika mkoa wa Mara utafuata kanuni na taratibu zilizowekwa na chama na kwamba kamwe hakutakuwepo na upendeleo wa aina yoyoye.

"Tunataka viongozi wenye hadhi, viongozi wenye uwezo wa kuongoza, viongozi wenye ushawishi na watakaoendelea kujenga heshima ya chama pamoja na kuisimamia serikali na viongozi hao wanapatikana kwa njia za haki bila kuwepo kwa mizengwe wakati wote wa uchaguzi," amesema.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live