Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Waliokuwa madiwani Chadema, ACT kugombea tena kwa tiketi ya CCM

11359 Udiwani+pic TanzaniaWeb

Sat, 14 Jul 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Babati. Chama cha Mapinduzi (CCM) mkoa wa Manyara kimewapitisha waliokuwa madiwani wa Chadema na ACT-Wazalendo kuwania tena udiwani kwa tiketi ya chama hicho tawala katika uchaguzi utakaofanyika Agosti 12, 2018.

Madiwani hao waliovihama vyama vyao na kujiunga na CCM siku za hivi karibuni, wamepitishwa na kikao cha halmashauri kuu ya CCM mkoani hapa.

Akizungumza na MCL Digital leo Ijumaa Julai 13, 2018, katibu mwenezi wa CCM Mkoa wa Manyara, Jacob Siay amewataja wagombea hao na kata zao katika mabano kuwa ni Nicodemus Tlaghasi (Bagara), Justin Masuja (Hayderer) na Paul Aweso (Tumati). Wote ni katika halmashauri ya wilaya ya Mbulu.

Wengine ni Mathayo Semhanda (Gehandu) na Marco Martin (Masakta) ambao kata zao zipo halmashauri ya wilaya ya Hanang. 

Soma Zaidi:

Wagombea CCM Manyara kujulikana Julai 12

 

 

Chanzo: mwananchi.co.tz