Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Waliofukuzwa CUF wamuangukia Msajili

Sakaya Waliofukuzwa CUF wamuangukia Msajili

Wed, 10 Nov 2021 Chanzo: ippmedia.com

WALIOKUWA viongozi katika Chama cha Wananchi (CUF) na kuvuliwa uongozi pamoja na uanachama wametangaza kwenda kwa Msajili wa Vyama vya Siasa nchini kudai kile walichokiita tafsiri ya uamuzi uliofanyika kutokana na ukiukwaji wa taratibu katika chama hicho zilizopelekea kuvuliwa uongozi na uanachama

Wakizungumza na vyombo vya habari Jijini Dar es Salaam jana, viongozi hao akiwemo Mkurugenzi wa zamani wa habari na uenezi, Abdul Kambaya ambaye alidai kuwa utaratibu uliotumika kuwavua uanachama haukufuata misingi ya Katiba ya chama hicho ikiwemo kutotimia kwa akidi ya wajumbe na kuingizwa kwa wajumbe wasiokuwa halali.

“Tutapelekea malalamiko yetu kwa Msajili kuomba tafsiri ya zile ibara zilizokiukwa ndani ya kikao cha baraza kuu, tunafanya haya kukinusuru chama na kulinda heshima ya chama chetu” alisema Kambaya.

Kambaya aliukosoa uongozi wa chama hicho kwa kile alichodai kutokubali kukosolewa na kufuata misingi ya Katiba wakati ambapo chama hicho kimekuwa kiitaka Serikali ya Chama cha Mapinduzi kufuata Katiba na kukubali kukosolewa jambo ambalo linawafanya kuonekana hawana msimamo.

Chanzo: ippmedia.com