Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Waliochukua fomu za Ubunge Ngorongoro wafikia 13

Nec3 1?fit=640%2C360 Waliochukua fomu za Ubunge Ngorongoro wafikia 13

Fri, 12 Nov 2021 Chanzo: Habarileo

WAGOMBEA wa vyama 13 vya siasa wamejitokeza kugombea ubunge katika jimbo la Ngorongoro katika uchaguzi mdogo unataraji- wa kufanyika Desemba 11 mwaka huu.

Uchaguzi huo mdogo unafanyika kufuatia aliyekuwa mbunhe wa jimbo hilo Willium Ole Nasha kufariki nyumbani kwake Jijini Dodoma Septemba mwaka 2021.

Kwa mujibu wa tarifa iliyotolewa na msimamizi wa uchaguzi wa jimbo la Ngorongoro Dk Juma Mhina aliwataja wagombea hao kuwa ni pamoja na Emmanuel Shangai (CCM) Simon Bayo (SAU) Singa Kalekwa (CCK), Amina Mcheka (NLD) Mary Daudi (UPDP).

Dk, Mhina aliwataja wagombea wengine kuqa ni Mgina Mustafa (AAFP), Frida Nnko (UMD), Paulo Makuru (UDP), Shafii Kitundu (ADC), Feruziy Feruziyson (NRA), Simon Ngil- isho (DEMOKRASIA MAKINI), Jonson Gagu (ACT WAZALEN- DO) na Zuberi Hamis (ADA TADEA).

Chanzo: Habarileo