Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Walemavu, wasiojua kusoma kusaidiwa kupiga kura

1f39cb591c50543bf498af0c862a3514 Walemavu, wasiojua kusoma kusaidiwa kupiga kura

Wed, 30 Sep 2020 Chanzo: habarileo.co.tz

KWA mara ya kwanza katika historia ya Uchaguzi Mkuu nchini, watu wenye mahitaji maalumu wakiwemo walemavu, watakwenda vituoni na wasaidizi wao kuwasaidia kupiga kura kumchagua Rais, wabunge na madiwani.

Makamu Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Jaji mstaafu Mbarouk Salum Mbarouk alisema lengo la hatua hiyo ni kuhakikisha watu wenye ulemavu wanatumia haki yao ya kikatiba kuchagua viongozi.

Alisema hayo alipozungumza na wadau wa uchaguzi kuhusu maandalizi ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka huu mkoani Dodoma Jaji Mbarouk pia alisema wasimamizi wa uchaguzi, wameelekezwa wawape kipaumbele wajawazito, wanaonyonyesha, wanaokwenda vituoni na watoto, wazee na wagonjwa.

“Kwa wale wasiojua kusoma na kuandika, wanaruhusiwa kwenda na watu wanaowaamini kwa ajili ya kupiga kura… kwa watu wenye ulemavu wa kutoona, kila kituo kati ya vituo 80,155 kitakuwa na vifaa cha maandishi ya nukta nundu kwa wale wanaoweza kutumia maandishi hayo na kwa wasioweza kusoma na kuandika wataenda vituoni na watu wanaowaamini,” alisema.

Alisema kwa wenye ulemavu wa viungo, vituturi (vikasha vya kupigia kura) vitakavyotumika vinaruhusu kuwahudumia, kwani vina pande mbili tofauti, upande mmoja kina urefu wa kuridhisha na kikigeuzwa kinakuwa kifupi kumwezesha mwenye ulemavu wa viungo kupiga kura.

Alisema NEC imejipanga kusimamia uchaguzi kwa kufuata misingi ya katiba, kanuni, sheria na taratibu ili uwe uchaguzi huru, wa haki, wa kuamilika kwa kuweka mazingira sawa ya ushindani kwa wagombea na vyama vyote vinavyoshiriki.

Chanzo: habarileo.co.tz