Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wajumbe wamgomea Dk Tizeba kuwa mwenyekiti wa uchaguzi

Tzeba Pic Data Wajumbe wamgomea Dk Tizeba kuwa mwenyekiti wa uchaguzi

Mon, 3 Oct 2022 Chanzo: Mwananchi

Mbunge wa zamani wa Buchosa, Dk Charles Tizeba amepata wakati mgumu, baada ya wajumbe 1,423 wa mkutano mkuu wa CCM wilaya ya Sengerema kumgomea kuwa mwenyekiti wa muda kwenye uchaguzi wa kuwachagua viongozi.

Hatua hiyo imekuja baada ya msimamizi wa uchaguzi Lameck Mahewa kuwaomba wajumbe wapendekeze jina la mwanachama moja kuwa mwenyekiti wa muda wa uchaguzi huo Jana Oktoba 2,2022.

Wajumbe hao baada ya Tizeba kupendekezwa waligoma kumpatia kura za ndiyo, huku wakimpendekeza diwani wa Kata ya Nyanzenda, Idama Kibanzi kuwa mwenyekiti wa muda kwenye kwenye uchaguzi huo.

Mmoja wa wajumbe hao, Amoni John amesema kila moja anaweza kuwa kiongozi siyo kutegemea watu wenye majina makubwa.

Dk Tizeba aliyekuwa Waziri wa Kilimo kabla ya kuenguliwa na Hayati Rais John Magufuli Novemba 2018, alikwama kwenye kura za maoni za uchaguzi wa mwaka 2020 baada ya Eric Shigongo ambaye sasa ni Mbunge wa Buchosa kupitishwa kugombea.

Chanzo: Mwananchi