Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Waitara aitwa ‘msaliti’ uzinduzi wa kampeni za Chadema

13874 KAMPENI+PIC TanzaniaWeb

Sat, 25 Aug 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Unaweza kusema Mwita Waitara amegeuka gumzo katika uzinduzi wa kampeni za Chadema katika jimbo la Ukonga jijini hapa kutokana na madiwani  wa chama hicho kikuu cha upinzani kulitaja jina lake kila wanapopanda jukwaani, kumfananisha na ‘msaliti’.

Julai 28, 2018 Waitara aliyekuwa mbunge wa Ukonga kwa tiketi ya Chadema tangu mwaka 2015, kuhamia CCM ambako amepitishwa na chama hicho tawala kuwania tena ubunge katika jimbo hilo.

Leo Jumamosi Agosti 25, 2018 Chadema wanazindua kampeni katika jimbo hilo, Waitara amekuwa akitajwa zaidi.

Diwani wa Kata ya Kitunda, Nice Gisunte amesema pamoja na Waitara kuhama Chadema, wanachama wa chama hicho hawapaswi kurudi nyuma.

“Sisi ndio tulimchagua Waitara na kumfanya kuwa mbunge na sisi ndio tutamwangusha,"amesema.

Diwani wa Kata ya Tabata, Patrick Asenga amesema marudio ya uchaguzi huo ni kipimo kwa wananchi kama wana uwezo wa kufikiri.

"Bado maisha magumu, barabara mbovu lakini mtu anatudanganya anaunga mkono jitihada, jitihada zipi,” amehoji.

Kwa upande wake diwani wa Ilala, Dorcas Mkiko amesema mwisho wa ubaya ni aibu, “unapiga kura,unalinda kura.”

Agosti 15, 2018 Waitara alifanya mahojiano maalum na MCL Digital na kujisifu kuwa alikuwa ‘jembe’ ndani ya Chadema  kwa kuwa ameshiriki kwenye chaguzi ndogo nyingi na harakati za chama hicho, akitoa mfano wa Jimbo la Igunga mkoani Tabora.

 

Chanzo: mwananchi.co.tz