Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Waitara: Magufuli chapa kazi usibabaishwe na maneno

32421 Waitarapic Tanzania Web Photo

Wed, 19 Dec 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Mbunge wa Ukonga(CCM), Mwita Waitara amemwambia Rais John Magufuli kufanya kazi na kutosikiliza maneno ya watu.

Naibu Waziri huyo wa Tamisemi ametoa kauli hiyo leo Jumatano Desemba 19, 2018 baada ya kupewa nafasi na Rais kuwasalimu wananchi katika hafla ya uwekaji jiwe la msingi la upanuzi wa barabara ya Morogoro jijini Dar es Salaam iliyofanyika eneo la Kimara Stop Over.

Upanuzi wa barabara unafanyika eneo la Kimara hadi Kibaha mkoani Pwani lenye urefu wa kilomita 19.2

”Uzuri hivi sasa wananchi wanakuelewa, hivyo piga kazi haya maneno ya watu yasikufanye ukafumba macho fanya kazi mimi mwenyewe nimeondoka huko (Chadema) kwa kuwa ni chama ambacho hakina shukrani,” amesema.

“Ni chama ambacho kwa kweli mbele za Mungu hakina shukrani kabisa. Nilitegemea mkuu wa mkoa (Paul Makonda-Dar es Salaam) wakati anataja mafanikio ya uboreshaji wa miundombinu ya elimu, wabunge (wa Chadema) wangesimama na kusifia lakini hawakufanya hivyo.”

Waitara amesema kwa niaba ya wabunge hao wa Chadema, amempa shukrani Makonda.

Aliongeza, “Nashangazwa na wabunge (wa Chadema) kuponda uboreshaji wa miundombinu ya barabara, kuna mmoja alisimama na kusema ‘wananchi watakula barabara’, nilitamani wananchi wa Ukonga wangekuwepo wakampiga mawe.”

Wakati Waitara akieleza hayo, Rais Magufuli alitumia uzinduzi huo kusisitiza upendo  kwa viongozi wote bila kubagua vyama vyao.

”Nawashukuru sana wabunge mliopo hapa huu ndiyo mshikamano tunaoutaka, tusibaguane sote ni wamoja tuchapeni kazi,” amesema.

Miongoni mwa wabunge waliohudhuria hafla hiyo ni mbunge wa Kibamba (Chadema), John Mnyika na mbunge wa Kinondoni(CCM), Maulid Mtulia.

 



Chanzo: mwananchi.co.tz