Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Waitara: Atakayemkwamisha Rais, ama zake ama zetu..

Image 606 1140x640 Waitara.png Waitara: Atakayemkwamisha Rais, ama zake ama zetu..

Thu, 27 Jul 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mbunge wa Tarime Vijijini Mwita Waitara, amesema wamejipanga vizuri kutekeleza Ilani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) na hadi sasa kwa majimbo yote mkoani Mara wamefikia asilimia 98.

Amesema uchaguzi wa mwakani wa serikali za mitaa watashinda kwa kishindo na uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika mwaka 2025 wamejipanga kufanya vizuri.

“Nawaomba watu wa Mara na Tanzania, Serikali ya Chama Cha Mapinduzi imeweka mipango ya kuona wananchi wanapata mali, barabara, elimu, afya na vijana kupata ajira, hakuna mtu yeyote ambaye anapita katikati kumkwamisha Rais Samia na tukimuona ama zake ama zetu,” amesema Waitara.

Amesema Rais Samia Suluhu Hassan yupo imara wanamuunga mkono na serikali ipo imara.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live