Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Waitara: Ahadi zangu Ukonga tayari zimeshafanyiwa kazi

17531 WAITARA+PIC TanzaniaWeb

Mon, 17 Sep 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Mgombea ubunge jimbo la Ukonga kwa tiketi ya CCM, Mwita Waitara amesema ahadi zote alizoahidi katika kampeni zitafanyiwa kazi na nyingine zimeshaanza kuonekana.

Akizungumza leo Jumamosi Septemba 15, 2018 katika mkutano wa kufunga kampeni za jimbo hilo, Waitara amewahakikishia wananchi kuwa Rais John Magufuli hafanyi maigizo katika kutekeleza ahadi zake.

Kuhusu Sh4 bilioni za mikopo kwa kinamama, vijana na walemavu amesema kwa sasa hazina riba hivyo ukikopa Sh500, 000 utairudisha hiyo hiyo.

Kwa vijana waliojiajiri kwa kuendesha bodaboda ameahidi atawaondolea adha ya kusumbuliwa na askari wa usalama barabarani kwani kazi hiyo imewainua wengi kimaisha.

“Mimi ni mbunge ninayejitambua, kero zote nazijua kwa majina na watu kama sisi, moja tunaita moja sio watu wa kupindisha maneno,” amesema

Amewaomba wananchi wasigombane na wanachama wa kawaida kesho katika kwenye uchaguzi bali ugomvi na manyangumi wanaokula fedha za chama.

Chanzo: mwananchi.co.tz