Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wagombea wawili wawili waitibulia CUF, DP Arumeru

Fri, 19 Apr 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Arumeru. Vyama tisa vimejitokeza kuchukua fomu za kugombea ubunge katika Jimbo la Arumeru Mashariki katika uchaguzi utakaofanyika Mei 19, huku utata ukiibuka kwa wagombea wa vyama vya CUF na DP.

Katika vyama hivyo, wamejitokeza wagombea wawili wawili wakiwa na barua za utambulisho.

Uchaguzi huo unafanyika baada ya Bunge la Jamhuri ya Muungano kumvua ubunge Joshua Nassari (Chadema) kwa kudaiwa kutohudhuria mikutano mitatu mfululizo ya bunge bila kutoa taarifa.

Msimamizi wa uchaguzi mdogo wa Jimbo la Arumeru Mashariki, Emmanuel Mkongo akizungumza na Mwananchi jana alisema wagombea ambao wamechukua fomu ni kutoka NCCR-Mageuzi, Chama cha Sauti ya Umma (Sau), African Democratic Alliance (Ada) na Tadea.

Wagombea wengine ambao wamechukua fomu ni kutoka vyama vya Demokrasia Makini, Alliance for Africa Farmers (AAFP), United People Democract (UPDP), Nation Reconstruction Alliance (NRA) na CCM.

Emmanuel alisema uchukuaji fomu na kurejesha utakamalika leo na Tume ya Uchaguzi itatangaza majina ya wagombea waliokidhi masharti.

Emmanuel alisema kuna changamoto ambazo zimejitokeza katika uchukuaji fomu kwa wagombea wa CUF na DP kujitokeza wawili wawili.

“Nimewarudisha waje na mgombea mmoja baada ya kukubaliana ndani ya vyama vyao kabla ya siku ya mwisho,” alisema.

“Baada kupitisha wagombea, kampeni zitaanza Aprili 20, kwa watakaofanikiwa kuteuliwa kabla ya uchaguzi kufanyika Mei 19 “alisema.

Mjumbe wa Mkutano Mkuu wa CUF, Abdalah Shaaban alikiri kuibuka mgogoro juu ya wagombea lakini akasema wameshangazwa na mgombea ambaye hajapitishwa na chama hicho kuchukua fomu.

“Sisi mgombea ambaye tumempitisha namkumbuka kwa jina moja la Dk George, huyu mwingine ambaye amekweda kuchukua fomu hatumtambui ila suala hili linashughulikiwa na chama” alisema.



Chanzo: mwananchi.co.tz